HabariMichezo

Simba wapata nafasi nyingine pesa za Rais Samia ?

Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa amesema kuwa ahadi ya Rais Samia Suluhu Hassan ya kununua kila goli la Simba SC na Yanga SC litakalofungwa kwenye mashindano ya Afrika inaendelea hadi mwisho wa mashindano.

Kauli hiyo ya Msigwa ni kama Simba wamepata nafasi nyingine ya kujirekebisha na kuondoka na mamilioni hayo ya Mhe. Rais baada ya kushindwa kufanya hivyo mbele ya Raja Casablanca.

Gerson Msigwa ameeleza katika kila mchezo ambao timu hizo zinazoiwakilisha Taifa zitacheza, kila goli watakalofunga kila timu itapewa shilingi miloni 5.

Mnyama Simba alikosa bahati ya kuvuna pesa za Rais Dkt. Samia baada ya kupoteza kwa goli 3-0 dhidi ya Raja CA huku ‘Lunyasi’ wakishindwa kutupia nyavuni hata bao la kufutia machozi.

Yanga waliondoka na milioni 15 kutoka kwa Rais Samia Suluhu Hassan kutokana na kufunga magoli matatu kwenye mchezo uliyomalizika 3-1 dhidi ya TP Mazembe.

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents