Habari

Simba yakubali kipigo cha goli 2-1 kutoka kwa Tanzania Prisons

Mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara kati ya Simba na Tanzania Prisons uliochezwa katika Uwanja wa Sokoine Mbeya, umemalizika kwa wekundu hao kukubali kipigo cha goli 2-1 dhidi ya maafande hao.

14938357_10154706795074339_5568749821845445599_n

Timu ya Simba ilianza kupata bao lake katika dakika ya 43 kupitia winga wake Jamal Mnyate akiunganisha krosi nzuri kutoka kwa Shiza Kichuya.

Katika kipindi cha pili dakika ya 48 Prisons walipata bao la kusawazisha kupitia Victor Hangaya baada ya kuunganisha mpira wa krosi uliopigwa na Kimenya. 

Prisons walipata bao la pili dakika chache baadaye kupitia mfungaji yuleyule wa goli la kwanza na kuufanya mchezo huo kumalizika wa 2-1.

Katika hatua nyingine timu ya Azam imeiadhibu Mwadui FC 4-1.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents