Habari

Simbachawene: Serikali haina nia mbaya na wananchi

Waziri wa nchi ofisi ya Rais tawala za mikoa na serikali za mitaa, George Simbachawene amesema kuwa dhamira ya Rais Dkt John Magufuli ni kuwatumikia wananchi na kuhakikisha maendeleo yanapatikana kwa Watanzania wote.

Simbachawene

Amezungumza hayo katika kipindi cha “TUNATEKELEZA” kinachoandaliwa na HABARI MAELEZO kinachorushwa na TBC 1. Alisema kuwa serikali ipo kwaajili ya kuwatumikia wananchi katika kila sekta na kutatua changamoto wanazokumbana nazo wananchi.

“Kupitia falsafa yetu ya hapa kazi tu tutahakikisha tunawaletea wananchi maendeleo katika ilani ya 2015 -2020 ya chama cha mapinduzi kilicho na serikali”, alisema Simbachawene.

Dk Simbachawene aliwahakikishia wananchi kuwa lengo la serikali ya awamu ya tano ni kuwatimizia wananchi ahadi ilizowaahidi kwakuwa wanayo dhamira ya kweli ya kuwatimizia wananchi.

Aliongezea kwa kusema kuwa Rais Magufuli ameamua kuleta mabadiliko ya kweli katika nchi, ambayo yanalenga kuwabana wabadhirifu na mali za umma na kurejesha nidhamu kazini jambo ambalo limeanza kuonekana katika ofisi mbalimbali za umma.

BY: EMMY MWAIPOPO

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents