Afya

Siri ya popo wanavyoishi na Corona yafichuka, fahamu zaidi

Wanasayansi wanasema wamechunguza vinasaba vya popo sita duniani.

Maisha yao yanajumuisha kidokezo cha vinasaba vyao vinavyowafanya kuwa na kinga ya kipekee inayowalinda dhidi ya virusi vya corona.

Watafiti wana matumaini kwamba taarifa hizo zitawasaidia kufahamu siri ya vile popo wanabeba virusi vya corona na kuvisambaza bila wao wenyewe kupata maambukizi.

Wanasema kuwa huenda hilo likatoa suluhu ya kudumu kusaidia afya ya mwanadamu wakati wa janga hili na hata siku za usoni.

Profesa Emma Teeling kutoka chuo cha Dublin amesema kuwa chembe za urithi walizochunguza zimewafanya kubaini kwamba popo wana mifumo maalum ya kinga.

Na kuelewa vile popo wanavyoweza kumudu virusi vya corona bila wao kupata maambukizi kunaweza kusaidia kupata tiba mpya ya ugonjwa wa Covid-19.

“Ikiwa tunaweza kuiga kinga ya popo dhidi ya virusi, unaweza kupata tiba,” ameiambia BBC News.

“Tayari imeshabadilika na kukua, kwahivyo sio kwamba uvumbuzi unaanza mwanzo. Sasa tuna vifaa vya kutuwezesha kuelewa hatua tunazohitajika kuchukua; tunahitajika kuvumbua dawa ili kufanikiwa.”

Profesa Teeling mwanzilishi wa mradi wa Bat1K project, unaopanga kuchunguza vinasaba vya spishi 1,421 za popo walio hai.

“Vinasaba hivi ndio vinavyohitajika kubaini suluhu ya kijenetiki inayotokana na popo ambayo hatimaye inaweza kuboreshwa na kuweza kukabiliana na magonjwa,” amesema.

Ugonjwa wa Covid-19 unasemekana kwamba chimbuko lake ni popo kulikosambaa hadi kwa mwanadamu na wao sasa kuanza kusambaziana.

Magonjwa mengine pia ikiwemo maradhi ya Sars, Mers na Ebola, pia yanasemekana kwamba yalifika kwa mwanadamu kwa njia hiyo hiyo.

Greater horseshoe bat
Wanaikolojia na wahifadhi wa mazingira wameonya kwamba popo wasiuliwe

Wanaikolojia na wahifadhi wa mazingira wameonya kwamba popo wasiuliwe au kuchukuliwa vibaya; kwasababu wanapoachwa wakiwa kwenye mahangaiko kwenye mazingira yao wanayoishi huenda wakasababisha hatari kidogo kwa afya ya mwanadamu.

Na pia ni muhimu kwa kuhakikisha urari wa asili duniani.

Wengi wao ni wachavushaji, wanatoa mbegu kutoka kwenye matunda na wengine ni wala wadudu ambao hula wadudu tani milioni kadhaa kwa usiku mmoja.

Ni spishi gani ya popo wanaochunguzwa?

Spishi sita za popo: ni popo aina ya horseshoe kwa Kiingereza jamii ya (Rhinolophus ferrumequinum), Egyptian fruit jamii ya (Rousettus aegyptiacus), popo kwa jina pale spear-nosed jamii ya (Phyllostomus discolor), Popo kwa jina greater mouse-eared jamii ya (Myotis myotis), popo Kuhl’s pipistrelle jamii ya (Pipistrellus kuhlii) na popo velvety free-tailed kwa Kiingereza jamii ya (Molossus molossus).

Utafiti umebaini nini?

Timu ya kimataifa ya watafiti inayotumia teknolojia ya kisasa inachunguza chembe za urithi za popo na vinasaba vyao vya sasa.

Kwa kulinganisha hilo dhidi ya wanyama wengine wanaonyonyesha 42 waliweza kujua maisha ya popo.

Popo wanaonekana kuwa karibu na kundi la wanyama walao nyama (mbwa na paka na spishi zingine), kakakuona, nyangumi na wanyama wenye kwato.

Kukokotoa utofauti wa jenetiki kulibaini chembe za urithi ambazo zimekuwa na mabadiliko tofauti kwa popo jambo ambalo huenda linachangia uwezo wao wa kipekee.

Kazi ya kuchunguza jenetiki zao ilibaini chembe ambazo huenda zinachangia mwangwi wa sauti zao ambayo popo hutumia kuwinda na kutembea kwenye maeneo yenye giza totoro.

Je taarifa hizo zitasaidia vipi kukabiliana na janga hili na mengine ya siku za usoni?

Kazi yao inaathari kwa afya ya mwanadamu na magonjwa kwa kubaini mabadaliko makubwa kwenye chembe za urithi ambayo yanatoa kinga kwa popo dhidi ya virusi.

Watafiti wanafikiria kuwa elimu ya chembe za urithi za popo kutasaidia kuelezea vile wanyama wanaonyonyesha wenye uwezo wa kuruka wanamudu maambukizi ya virusi vya corona, siku za usoni kutasaidia kukabiliana na janga.

“These changes may contribute to bats’ exceptional immunity and points to their tolerance of coronaviruses,” said Dr Michael Hiller of the Max Planck Institute of Molecular Cell Biology and Genetics in Dresden, Germany.

“Mabadiliko haya huenda yanachangia popo kuwa na kinga ya kipekee na kuangazia uwezo wao wa kukabiliana na virusi vya corona,” amesema Dkt. Michael Hiller wa Taasisi ya Max Planck ya masuala ya Biolojia na Jenetiki huko Dresden, Ujerumani.

Katika maambukizi mengi yanayosambaa, sio virusi pekee vinavyochangia kifo, lakini pia uvimbe mkubwa kunakotokana na mfumo wa kinga ya mwili.

Popo wanaweza kudhibiti hili. Kwahiyo, ingawa pengine huenda wanaweza kupata maambukizi, hawaoneshi dalili za ugonjwa wenyewe.

Utafiti huu umechapishwa kwenye jarida la Nature.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents