Burudani

Stopa Rhymes adai hatoachia tena audio bila ya video

Msanii wa Hip Hop Bongo, Stopa Rymes amedai kuwa kwa sasa amepata menejimenti nzuri ya Scorpion Entertainment yenye studio ya kurekodia na kampuni ya production hivyo hatoweza tena kukaa kimya kwa kuachia audio bila ya video

stoppa (1)

Akiongea na mtangazaji Dj Magasha kwenye kipindi cha Track 2 Track cha Fadhila FM ya Masasi, Stopa amesema kuwa kwa sasa tatizo la kuachia audio bila ya video halitatokea tena.

“Sikuwa nimefanya video kwa wakati fulani, juzi kati tulienda kufanya maandalizi ya video. Kuna nyimbo zimeshafanyiwa video hata hiyo na tumeshafanya video ya wimbo wa Hardcore Hip Hop’ ambao nilikuwa nimeuachia siku za karibuni. Kutakuwa na muendelezo wa kuachia video nyingi kwa sababu sasa hivi nipo chini ya menejimenti inayomiliki studio na kampuni ya video production. Kwahiyo kwa sasa suala la video litakuwa tofauti na siku za mwanzo,” alisema Stopa.

“Video inasaidia ile vision kwa sababu watu wanakuwa wanasikia nyimbo lakini kukuona pia inakusaidia kwa kuwa wanaiona image yako ila watu wengi wanapenda kukuona zaidi kwa sababu wakikuona unakuwa unawavutia watu. Video kwa sasa ipo kwenye catalog watu wanapenda kuona video zaidi kuliko kusikiliza audio,” aliongeza.

Msikilize Stopa hapo chini.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents