Habari

Damian Soul asimulia jinsi ngoma yake Kaumba aliyomshirikisha Vanessa Mdee ilivyomtoa jasho (Video)

Damian Soul amesema wimbo wake ‘Kaumba’ aliomshirikisha Vanessa Mdee ulimtoa jasho haswaa – kama sio kamasi kabisa.

4K0A8812

Amedai kuwa wimbo huo ulizaliwa alipokuwa nchini Kenya mwaka jana kwenye kipindi cha Maisha Superstars. Anasema alitaka kufanya wimbo na Nameless aliyemwambia kuwa anaupenda sana wimbo wake ‘Dua la Kuku’ kiasi cha kumshawishi waufanyie kitu lakini alishauri wafanye kitu tofauti.

Anasema ndipo walipoenda kwa producer Sappy na kuanza kukuna kichwa kutengeneza wimbo wao hadi pale walipopata idea ya Kaumba na wakawa na beat chorus. Aliporudi Dar alianza kuufanyia kazi wimbo huo ikiwemo kuandika mashairi na katika moja ya mazungumzo na Joh Makini alisaidiwa kupata mistari ya kwanza iliyomshawishi kumalizia kuandika.

Alimtumia wimbo huo Vanessa kumuomba amshirikishe na Vee anadai aliupenda tu alipousikia mara ya kwanza.

“Nilikuwa nausikiliza nikiwa naenda Nigeria nikaweka hiyo song on replay nikalala hivi, I am telling you nilikuwa nashindwa kulala,” anasema Vanessa.

Hicho kilimpa moyo Damian na kudai kuwa hakuna kitu kizuri kama mtu unayetaka kumshirikisha akiupenda wimbo na sio kukubali kufanya kwasababu ya heshima.

“I was very happy aliposema ameupenda,” anasema Damian.

Damian anadai kuwa baada ya Sappy kuja Dar alimpa file la wimbo huo ulipofikia na kwenda nalo kwa Nahreel na kuongeza vionjo vingine vilivyouboresha zaidi wimbo huo. Hata hivyo baada ya wimbo huo kukamilika, Vanessa hakupenda ubora wake na kumrudisha Damian studio.

“Ukweli siku hiyo nilitamani nilie kidogo,” anasema Damian.

“Damian kaniletea wimbo kaumaster nikamwambia not yet, bado nyimbo ni kubwa kwanini unaipa mastering ndogo, mimi mwenyewe naona kama nimeimba vibaya, tukaanza upya tukafuta yote,” ameongeza Vanessa.

Wanasema version ya Kaumba inayosikika sasa ni kama ya sita kurekodiwa.

Haikuwa rahisi baada ya hapo, Damian anasema. Ilimlazimu kulala studio kwa takriban siku tatu kusubiria kuufanyia marekebisho wimbo huo. Anasema mtu aliyerekodi naye wimbo huo alimwambia Damian kama angekuwa na kamera angerekodi jinsi alivyousotea wimbo huo. Anadai alimuomba radhi kwa jinsi alivyomtesa siku zote hizo kutokana na kuwa na ratiba ngumu.

“Kwahiyo unakaa pale unamsubiri, ‘nakuja’ masaa sita nasema this song has to be done today, unalala unaamka asubuhi kwenye kochi, ‘sorry sasa Damian wewe nenda’ niende wapi mimi, sijaoga hapo almost three days nipo tu around mpaka gari imepaki nje chafu mpaka yule owner wa studio ananiambia ‘Damian haki ya mama’ lakini at the end of the day we got something ambacho sasa hivi watu wanafurahia.”

Damian anadai kuwa ‘Kaumba’ ni wimbo spesho sana kwake kwasababu ndio wa kwanza kumshirikisha msanii wa kike tena mkubwa kama Vanessa Mdee.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents