Habari

Suma Mnazareth Amlipua Ustaadh Juma!


Msanii wa nyimbo za kufoka foka nchini Suma Mnazareth ambaye alikuwa memba wa kundi la watanashati jana jioni alitoa ya moyoni kuhusu uhusiano wake na crew yake ya zamani ya Watanashati pamoja na uhusiano wake na Boss wa label hiyo Ustaadh Juma.
Suma Mnazareth aliyazungumza hayo wakati akifanya mahojiano katika kipindi cha 5 selekt kinachoruka katika kituo cha Televisheni cha East Africa. Alianza kuongelea namna ambavyo aliingia katika lebo hiyo ambapo alidai alijiunga na watanashati baada ya kurekodi nyimbo yake ya kwanza na katika kutafuta meneja ambaye atamsaidia kufanikisha ndoto zake za kisanii Ustaadh Juma alimkubali na kukubaliana watafanya kazi pamoja.

“Mimi sikwenda watanashati kama mtu ambaye alikuwa hana pa kuanzia ila nilianza kufanya kazi nao nikiwa na nyimbo yangu “Chukua time” tayari ya ambayo ilitengenezwa na prodyuza Manek na kumshirikisha Ommy Dimpoz. Ki ukweli Ustaadh Juma alinisaidia kwa kulipia video ya wimbo huo na kuchangia laki moja na nusu kwenye pesa ya lokesheni ambayo ilikuwa laki mbili’.

Akiongelea namna ambavyo ameondolewa katika kundi hilo Suma alisema yeye anavyojua Ustaadh Juma amemtoa kutokana na majungu na fitina na kwambameneja wake huyo alikuwa anawasikiliza watu wa pembeni kwani anao wapambe wengi ambao kila mmoja anasema kwake.
Ugomvi wa juzi juzi ambao unasemwa mimi nilizinguana na PNC umekuzwa kwani haukufikia hatua mbaya hivyo, kila mtu anajua namna suma mnazareth alivyo jina kubwa si Tanzania tu bali hata afrika kusini. Mimi kwenye kundi nimepitia wakati mgumu kwani ushirikiano haukuwa mzuri sana kutokana na mikwaruzano ya mara kwa mara.

Akiendelea suma alisema anajua hujuma ambayo ustaadh Juma atamfanyia kwani alishawahi kufanya hivyo wakati yeye yu ndani ya kundi .jamani watanzania naomba mnisikilize kwa makini. “Wakati nipo watanashati Ustaadh juma aligombana na msanii mmoja na baada ya kumtema, Ustaadh juma alikuwa anapiga simu kwenye mtandao wake wa watu wa media kuanzia watangazaji, ma dj na kadhalika na kuwataka wasipige nyimbo zake sasa najua zamu yang undo hiyo imefika alisema Suma mnazareth kwa kujiamin”. Alisema Ustaadh Juma sio mtu mzuri kabisa.

Naye Ustaadh Juma akiongea kwa njia ya simu na watangazaji wa kipindi cha 5 Selekt alisema sababu kubwa ya yeye kumtema suma mnazareth ni nidhamu mbovu pamoja na kutozingatia mambo muhimu ya kimaendeleo. Akiendelea Ustaadh alisema suma amekuwa na tabia ya ulevi wa kupindukia na kwamba watu walimuonya wakati akimchukua kwenye lebo yake lakini hakuwasikiliza mpaka alipojionea mwenyewe.

Huwezi kuwa na msanii ambaye anataka kula bata wakati haingizi chochote kwani pesa inabidi itafutwe sasa mwenzangu yeye anapenda sana starehe na akilewa anakuwa mgomvi.Mi nimepigiwa simu na watu pale studio ebana hebu njoo umuone msanii wako analeta fujo mi nikasema siendi kama mambo yenyewe ndio hayo kwani ninawatu wananiheshimu.
Alipoulizwa kama alikuwa na mkataba na Suma Mnazareth Ustaadh alisema mimi nilimuweka kwanza kwa majaribio na hakuweza kukidhi vigezo. Mbona hawa wasanii wengine nina mkataba nao. Alijibu Ustaadhi juma.

Akiendelea na mahojiano baada ya maneno hayo ya Ustaadh Juma, suma mnazareth alisema maadam ametoka kwenye lebo hiyo hana kinyongo zaidi na kwamba hawezi kuwa mchoyo wa fadhila kwa yale mazuri ambayo amefanyiwa ila lebo ya watanashati wasijifanye wanataka kumbania kazi zake ambazo hazikutokana na nguvu yao na wamwache afanye kazi kivyake kwani wakithubutu anao wanasheria wanne wa kumtetea.

Wakati huo huo aliyekuwa meneja wa Watanashati bwana Maneno amefunguka kwa kukanusha maneno yaliyokuwa yamesambaa kuwa na yeye ni mmoja wa waliofukuzwa na kusema yeye ndiye aliyemuomba bosi wa Watanashati Ustaadh Juma kuacha kazi.” Mimi sikufukuzwa na mtu yeyote ila niliomba mwenyewe na kwamba sikuweza kufanya kazi na mtu ambaye naona hakitambui ama haelewi anataka nini”.
Haya sasa picha ndo limeanza.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents