Bongo Movie

Jackline Wolper kuanza kutengeneza filamu zake mwenyewe


Baada ya muigizaji mkongwe Hashim Kambi kuanza kutayarisha filamu zake mwenyewe, Jackline Wolper naye ameunga tela.
Muigizaji huyo mrembo amesema kupitia kampuni ya JB Production, ataanza kuandaa filamu zake.
Katika azma hiyo, Wolper atasaidiwa na meneja wake Leah Mwendamseke aka Lamata.
Vyanzo vimedai kuwa tayari kampuni hiyo imekamilisha kurekodi filamu iitwayo Malipo ni Hatari.
“Nimeingia katika fani ya utayarishaji na kwa kuanza ninakuja na filamu ya Malipo, ni filamu ya kipekee kuanzia hadithi, waigizaji wake wameigiza katika kiwango kikubwa cha kimataifa , okay sisemi mengi bali mtaona katika filamu ya Malipo,” Jack aliuambia mtandao wa Filamu Central.
Miongoni mwa waigizaji walioshiriki kwenye filamu hiyo ni pamoja na yeye mwenyewe, Blandina Chagula ‘Johari’, Stanley Msungu ‘Seneta’, Hashim Kambi ‘Ramsey’, Fatuma Makongoro ‘Bi. Mwenda’, Mgata, Ahmed Ulotu ‘Mzee Chilo, Slim na wengine.
Malipo ni Hatari imeongozwa na Lamata.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents