Burudani

Super Soul Sunday: Unayopaswa kufahamu pindi unaposhindwa

kama ilivyokawaida kila Jumapili nakusongezea hizi nukuu saba kutoka kwa watu ambao wamefanya mambo makubwa au ya kipekee katika dunia hii. Nukuu za leo zimelenga kukuinua pale unaposhindwa (failure) katika jambo fulani pindi unapoelekea mafanikio yako.

  1. Watu waliofanikiwa hunufaika katika makosa yao kwa kuwa hujaribu tena katika njia nyingine – Dale Carnegie.
  2. Aliyeshindwa pekee ndio huwa hajaribu – Anna Kleimer.
  3. Kushindwa ndio fursa pekee ya kuwa jasiri tena – Henry Ford.
  4. Kosa kubwa zaidi ambalo mtu anaweza kutenda, ni kuhofia kufanya tena – Elber Hubbard.
  5. Ni kweli siwezi kukupa njia sahihi ya mafanikio lakini nakupa njia ya kushindwa, nayo ni kurajibu kuomba samahani kwa kila mmoja – Bernard Meltzer.
  6. Kushindwa ni mafanikio kama utaamua kujifunza katika hilo – Malcolm S. Forbes.
  7. Hakuna kushindwa kwa yule anayefanya kilicho bora – Orison Swett Marden.

Shukrani, dondosha comment yako hapo chini kuelezea ni nukuu ipi imekubamba zaidi.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents