Bongo5 Makala

Makala: Mafanikio ya Alikiba kimuziki mwaka huu, 2017

Rais wa 16 wa Marekani kati ya mwaka 1861 hadi 1865, Abraham Lincoln alipata kutoa msimamo wake kwa kile anachokiamini kitamfanya kufikia malengo yake. Lincoln alisema, “Ninafanya vizuri kwa namna ninavyojua na ninaweza kuwa bora, ninamaanisha nitaendelea kufanya hivyo hadi mwisho”.

Kwa lugha nyepesi mithili ya nyoya katika anga ni kwamba Abraham Lincoln aliamini katika jitihada zake na utashi pekee ndizo zitamfikisha pale anapoahitaji kufika ili kuwa bora kitu ambacho anakula kiapo kufanya hivyo hadi tamati.

Karibu Alikiba

Hakuna asiyetambua uzito wa jina lake katika muziki wa Bongo Flava, kutokana na hilo sitoona gharama kuinua mkono wangu na kuandika machahe yenye utoshelevu kuhusu mafanikio yake kimuziki kwa mwaka huu, 2017 ambao upo mbioni kumalizika.

Kwa mwaka 2017 Alikiba ameishi katika maneno ya Abraham Lincoln ‘ninafanya vizuri kwa namna ninavyojua na ninaweza kuwa bora’.

Wakati tukizungumzia mafanikio ya Alikiba kwa mwaka 2017, utakumbuka ni mwaka ambao unaelekea kuisha akiwa ametoa ngoma yake moja tu official kitu ambacho naona ni kama mfumo wake, hata hivyo ameweza kuwa bora. Haya ni maeneo ambayo amefanikiwa kwa mwaka huu.

  1. Boss RockStar4000

July 4 mwaka huu Rockstar4000 walimtangaza Alikiba kuwa ni miongoni mwa wamiliki wa kampuni ya Rockstar4000 Music Entertainment Co & Rockstar Television. Msanii huyu ambaye amekuwa chini ya RockStar400 kwa miaka sita pia atakuwa Director of Music and Talents.

Utakumbuka awali Alikiba alikuwa msanii wa kawaida chini ya RockStar4000 pamoja na Lady Jadee na Barakah The Prince ambao kwa sasa hapo tena katika label hiyo.

Alikiba kufikia mafaikio yake ni hatua kubwa amepiga katika muziki wake kwani amekuwa akifanya kazi chini ya RockStar4000 kwa kipindi kirefu sasa, kuna wasanii wengine wangeweza kuchukua nafasi hiyo lakini imetua mikononi mwake si kwa bahati mbaya ila uwezo wa kazi.

B. Ujio wa King’s Music

Licha Alikiba kufanya kazi na Rockstar4000, pia ana label yake ‘King’s Music’. Label hii alitangaza ujio wake kwa kipindi kirefu lakini haikuweza kuja na kazi yoyote, hata hivyo mwaka huu imefanya kitu.

Msanii wa kwanza kutoa kazi chini ya King’s Music ni Abdu Kiba ambaye hivi karibuni ameweza kutoa ngoma mpya ‘Single’ akimshirikisha Alikiba. Bila shaka mwakani tutarajie wasanii wengine wakija na kazi zao chini ya label hiyo.

Alikiba kuja na label anaungana na msanii mwenziye, Ommy Dimpoz ambaye wapo wote RockStar4000 kumiliki label. Dimpoz kupitia PKP kwa sasa anamsimamia msanii mmoja, Nedy Music.

  1. Ushindi tuzo za AFRIMA

Usiku wa kuamkia November 13 mwaka huu Alikiba alishinda tuzo mbili za All Africa Music Awards 2017 (AFRIMA) ambazo hutolewa nchini Nigeria.

Alikiba alishinda katika vipengele vya Best Africa Collaboration kupitia ngoma ‘Aje’ pamoja na kipengele cha Best Artist or Group in Africa RnB and Soul ambapo pia ni kupitia ngoma ya ‘Aje’ kwa kushirikiana na M.I.

Msanii mwingine wa Tanzania aliyeshinda tuzo hizo ni Nandy akishinda katika kipengele cha Best Female Artist In Eastern Africa Award. Hivyo basi katika orodha ya washindi kutoka Bongo Alikiba anaongoza akifuatiwa na Nandy, huku Feza Kessy, Diamond, Lady Jaydee na Vanessa Mdee wakiondoka mikono mitupu.

B. Chukua hii

Pia mwaka huu February 17 ndipo Alikiba alikabidhiwa tuzo yake ya MTV EMA ambazo zilitolewa mwaka jana. Sababu ya Alikiba kupewa tuzo hiyo mwaka huu ilitokana na Wizkid kutangazwa mshindi ilhali kwenye website ya tuzo hizo, kura zilionesha Alikiba ndiye mshindi.

Baada ya MTV EMA kujua makosa yao, waliamua kumpokonya tuzo ya Best African Act Wizkid na kumpa Alikiba ambaye alistahili kushinda.

  1. Heshima kutoka Sony Music Africa

Pia mwaka huu Label ya Sony Music Africa, ilimtunuku tuzo Alikiba baada ya video ya wimbo wake Aje kufikisha views milioni 5 kwenye mtandao wa YouTube. Alikiba alipewa tuzo hiyo Johannesburg, Afrika Kusini ambapo ndipo yapo makao makuu ya Sony Music Africa.

Aje ilikuwa ngoma ya kwanza kwa Alikiba kutoa chini ya Sony Music Africa, kipindi ilipotoka iliweza kufikisha views milioni 1 ndani ya siku saba katika mtandao wa YouTube. Hiyo haijawahi kutokea kwa msanii yeyote wa Afrika aliyefikisha idadi hiyo ya views ndani ya kipindi hicho.

Hivyo hadi kufikisha views milioni tano ilikuwa ni hatua kubwa yenye kuhitaji pongezi na Sony Music Africa hawakukawia kufanya hivyo. Ngoma hiyo hadi sasa ina views milioni 7.3 tangu kuwekwa YouTube May, 19, 2016.

Baada ya hapo Alikiba alisema kuwa CEO wa Sony Music Africa, Sean Watson, ameiambia bodi ya label hiyo jinsi Alikiba alivyo na mashabiki wengi nyuma ambao panapotokea kuchelewa kwa lolote, ‘hung’ata kama nyuki, hivyo wasichelewe kutoa kazi.

Hayo ni machache niliyofanikiwa kukusanyia katika yale mengi mazuri aliyofanikisha Alikiba kwa mwaka huu, 2017. Naomba kuwasilisha.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents