Michezo

Taifa Stars kuvaana na Malawi leo

Timu ya taifa, Taifa Stars leo inatarajiwa kutupa karata yake ya kwanza ya kuwania ubingwa wa mashindano ya Kombe la Cosafa kwa kuikabili Malawi katika mechi ya Kundi A itakayopigwa leo saa 10 jioni jijini Johanesburg, Afrika Kusini.

Taifa Stars

Taifa Stars ambayo ipo kundi moja na timu ya Taifa ya Angola, Malawi na  Mauritius inashiriki kwa mara ya tatu michuano hiyo ya kila mwaka katika Ukanda wa nchi za Kusini mwa Afrika.

Baada ya mechi ya leo, Stars itashuka tena dimbani kesho kutwa kuikaribisha Angola na itamaliza mechi za hatua ya makundi kwa kuvaana na Mauritius  Juni 29, mwaka huu.

Kwa upande mwingine Kocha mkuu wa Taifa Stars, Salum Mayanga amesema atajitahidi kila liwezekanalo Taifa Stars ifanye vizuri kwenye michuano hiyo ya COSAFA kwani ni sehemu ya maandalizi yamichuano ya CHAN inayotarajiwa kutimua vumbi mwezi ujao.

Tunataka kufanya vizuri katika mashindano haya, lakini pia ni muhimu kuimarisha kikosi chetu kwa ajili ya michuano ya CHAN ambayo iko mbele yetu,” amesema Kocha wa Stars Salum Mayanga.

Katika michuano ya CHAN, Stars itacheza mechi yake ya kwanza nyumbani dhidi ya Rwanda (Amavubi) Julai 14, mwaka huu na Julai 21 itaifuata Amavubi  jijini Kigali kwa ajili ya mechi ya marudiano.

By Godfrey Mgallah

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents