Burudani

Tangu ameondoka Nahreel heshima ya Home Town Record imeshuka – Elly da Bway

Uongozi wa Home Town Record umekiri kushuka kwa heshima ya studio hiyo tangu aondoke aliyekuwa producer wa studio hiyo, Nahreel.

IMG_4627-3-1

Nahreel ambaye alifanya kazi kwenye studio hiyo kwa kipindi kirefu na kufanikiwa kufanya hit kadhaa na wasanii wakubwa kabla ya kuondoka na kuelekea Switch Record na sasa anamiliki studio yake ya The Industry Music ambayo imefanikiwa kutoa hit kibao ndani ya muda mfupi tangu imeanza.

Akizungumza na Bongo5 , producer wa studio hiyo, Elly da Bway amesema ‘Tunapanga kufanya kitu kikubwa ambacho kitarudisha heshima ya Home Town’.

“Unajua tangu aondoke Nahreel heshima ya Home Town imeshuka. Uongozi unajipanga kufanya kitu ambacho kitawafanya wasanii wengi waje kufanya kazi hapa. Hata hivyo nimeshaanza kupata dili na baadhi ya wasanii naona umeanza kuwa mwanzo mzuri na neema pia kwa studio na uongozi,” aliongezea.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents