Habari

TANZIA: Mzee Ndesamburo afariki dunia

Mbunge wa zamani wa Moshi Mjini (Chadema) Philemon Ndesamburo amefariki dunia ghafla leo, wakati akipata matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya KCMC, Moshi.

Mzee Ndesamburo

Katibu wa Chadema, Mkoa wa Kilimanjaro, Basil Lema amethibitisha kifo hicho na kueleza kuwa wataendelea kutoa taarifa zaidi juu ya kifo cha mwanasiasa huyo mkongwe.

Mzee Philemon Kiwelu Ndesamburo alizaliwa February 19, 1935. Alikuwa mwanasiasa kupitia chama cha demokrasia na maendeleo(CHADEMA) pia kufadhili mambo mengi kupitia chama hicho.

Mwaka 2000 alifanikiwa kuchaguliwa na wananchi wa Moshi mjini kuwa mbunge wao mpaka mwaka 2015 alipoamua kwa ridhaa yake kutogombea tena jimbo hilo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents