Habari

IGP Sirro atangaza dau nono kwa atakae toa taarifa ya mauaji Rufiji

Mkuu mpya wa Majeshi, IGP Simon Sirro ametangaza dau nono la Shilingi milioni 10 kwa atakayetoa taarifa kuhusu mauaji ya Kibiti, Rufiji na Mkuranga mkoani Pwani.

IGP Sirro akizungumza kwa mara ya kwanza na wanahabari leo, Makao makuu ya Jeshi la Polisi Dar es salaam amesema kuwa maneno yatakuwa machache kuliko vitendo.

“Niwaambie ukweli kuwa katika hili, maneno yatakuwa machache lakini vitendo vitakuwa vingi zaidi,” amesema katika mkutano huo. Atakayesaidia kukamata watu wanaousumbua huko Kibiti, Mkuranga, Rufiji mimi kama IGP nitatoa milioni 10 kwa mtu atakayefanikisha,” alisema IGP Sirro.

Mkoa wa Pwani umefululiza kutokea kwa matukio mbalimbali ya kihalifu ikiwa ni pamoja na viongozi mbalimbali kuuawa na watu wasio julikana.

Na Emmy Mwaipopo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents