Michezo

TASMA watangaza mchakato wa uchaguzi

Kamati ya uchaguzi ya Chama cha Wataalamu wa Tiba za Michezo (Chawatimita-Tasma) imetangaza kuanza rasmi kwa mchakato wa uchaguzi Mkuu wa chama hicho unaotarajiwa kufanyika Agosti 5, mwaka huu jijini Dar es Salaam.

M/mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya Tasma, Francis Mchomvu (kushoto),mwenyekiti wa kamati, Leslie Liunda,Ofisa Habari wa TFF, Alfred Lucas na mjumbe wa kamati, Ombeni Zavara

Mwenyekiti wa kamati hiyo, Leslie Liunda, amesema kesho Julai 7, fomu zitaanza kutolewa katika ofisi za Tasma zilizopo kwenye Chama cha Paralympic zilizopo karibu na Uwanja wa Uhuru na mwisho ni Julai 16, mwaka huu.Uchaguzi huo unahusisha nafasi ya Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti, Katibu Mkuu, Katibu Mkuu Msaidizi, Mweka hazina, Mjumbe wa mkutano mkuu TFF na wajumbe wawili wa kamati ya utendaji.

Huku gharama za fomu kwa wagombea wa nafasi ya wajumbe ni Sh 100,000, huku nafasi zingine gharama yake ikiwa ni Sh 200,000.

By Hamza fumo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents