Habari

TBA watoa maelezo kuhusu mabweni mapya ya UDSM yaliyopata nyufa

Mkurugenzi wa Wakala wa Majengo nchini, Mhandisi Elius A. Mwakalinga, amekiri wazi kuwa picha zinazosambaa mitandaoni zikionyesha majengo mapya ya mabweni ya Chuo Kikuu cha Dar es salaam (UDSM) kuwa na nyufa ni za majengo hayo, huku akiwatoa wasiwasi wanafunzi kwa kusema ni kitu cha kawaida kwa majengo makubwa.

Mwakalinga amesema kutokea kwa nyufa hizo ni moja ya hatua za ‘Expansion Joint’ ambazo hutumiwa kwenye ujenzi wa majengo huku akidai kuwa majengo hayo yamekidhi vigezo vyote vya vipimo wakati wa ujenzi wake.

Kila design tunayofanya ya majengo sasa hivi tunatumia Expansion Joint, majengo mengi makubwa huwa inatumia hiyo, hivyo ni common na sio creck kubwa sana kama inavoonekana kwenye picha, nilienda ile jana usiku kukagua tukakuta hiyo hali, ni process za majengo ili yaweze kusatle, hivyo watu wawe na amani kabisa wala wasiwe na hofu.“amesema Mwakalinga.

Kwa upande mwingine, Mwakalinga ametoa onyo kwa watu wanaosambaza picha hizo bila kupata ufafanuzi wa kitaalamu kutoka TBA wanafanya makosa kwani wanawatia watu hofu kwa jambo la kawaida kwenye hatua za ujenzi.

Chanzo:EATV

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents