Habari

TBS yawahimiza wahandisi na wananchi kuzingatia umuhimu wa viwango

Shirika la viwango Tanzania, TBS limewahimiza wahandisi wa kada mbalimbali kuzingatia umuhimu wa viwango vya ubora katika miradi wanayoisimamia ili kuhakikisha kwamba matokeo ya miradi hiyo inadumu kwa muda mrefu.

8-9

Afisa uhusiano wa shirika la TBS, Neema Mtemvu, ametoa msisitizo huo wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye maonesho ya wahandisi Tanzania yaliyofikia tamati Ijumaa hii jijini Dar es Salaam.

Aidha Afisa huyo alitoa sababu ya wao kuwepo siku ya wahandisi na lengo la wao kuwa pale na kutoa baadhi ya masomo kwa wananchi na wakandarasi kujua umuhimu wa viwango nchini.

“TBS tumekuja kwenye haya maonesho kwanza kabisa sisi ni wadau,kwasababu pale TBS sisi tuna viwango vya engineering kama viwango vya simenti,nondo, misumari,kwahiyo kwa kifupi tuna maabara pale tunapima,” alisema.

“Kwahiyo tumekuja hapa kuonana na maengineer sio tu maengineer hata wananchi kwa ujumla ili tuweze kuwapa elimu kuhusu viwango, umuhimu wa kupata leseni ya TBS ili waweze kufanya biashara za ndani na nje ya nchi,”, alisema Mtemvu.

BY:EMMY MWAIPOPO

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents