Habari

TCAA mshindi wa pili tuzo mwajiri bora wa mwaka 2023

MAMLAKA ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), imeibuka kuwa mshindi wa pili katika upande wa taasisi za umma kwenye kinyang’anyiro cha Tuzo za Mwajiri Bora kwa mwaka 2023 iliyoandaliwa na Chama cha waajiri Tanzania (ATE).

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana Desemba 4 2023 baada ya kupokea Tuzo hiyo katika hafla ya utaoji wa Tuzo za Mwajiri Bora ,Mkurugenzi Mkuu wa TCAA, Hamza Johari alisema TCAA inafuraha kuibuka katika miongoni mwa washindi kutoka katika Upande wa taasisi za umma ambapo itakuwa chachu kwao katika kuhakikisha wanaboresha mifumo Yao.

Alisema kupitia tuzo hizo watahakikisha mwakani wanafanya vizuri zaidi na kuibuka kuwa kidedea katika kuzidi kuboresha mifumo yao.”leo tulikuwa na mashindano ya kumtafuta mwajiri bora kwa mwaka 2023, jumla ya Taasisi 1000 zilishiriki katika kinyang’anyiro hiki lakini baadae 91 tu zilipitishwa kwenye hatua ya kwenda kupekuliwa na kukaguliwa zaidi kuona namna kama vile walivyojaza katika madodoso yapo sawa lakini baadae taasisi 14 tu zilienda katika hatua ya mwisho na kupatikana kwa mshindi kati ya hizo ya kwetu pia imekuaje miongoni mwao,”alisema.

Alisema kwa mwaka 2023,TCAA imefanya mambo mbalimbali ikiwemo kuimarisha mifumo ya kusimamia rasilimali na sera nzuri za kusimamia rasilimali watu katika kuhakikisha mikakati mbalimbali ya imewekwa katika kutekeleza sera za rasilimali za watu.

Johari alisema miongoni mwa sera za rasilimali za watu zinazotekelezwa ni pamoja na masuala ya maslahi ya wafanyakazi kuyaweka vizuri kuhakikisha wafanyakazi wanakuwa na hali na morali na taratibu zote.

“Wananchi watarajie huduma bora kwa sababu tuzo hizi zitaongeza chachu yakuendelea kufanya kazi vizuri tunashukuru ate kuandaa mashindano haya,”alisema.

written by Janeth Jovin

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents