Michezo

Tetesi za soka barani Ulaya Ijumaa hii, Zidane aridhishwa na Bale, Spurs kumsajili Dybala 

Tottenham itapewa nafasi nyingine ya kumsajili mshambuliaji wa Juventus Paulo Dybala, 25 mbaye thamani yake inakadiriwa kuwa £65m-dirisha la uhamisho wa wachezaji litakapofunguliwa tena mwezi Januari mwaka. (Star)

Atletico Madrid wanapigiwa upatu wa kumnunua kiungo wa kati wa Tottenham na Denmark Christian Eriksen, 27, Januari mwaka ujao. (Express)

Juventus inamtaka Kipa wa Manchester United David de Gea, 28, na wachezaji wengine wa klabu hiyo Eric Bailly, 25, na Nemanja Matic, 31, huenda ikiweka dau la kuwanunua msimu ujao. (Gazzetta Dello Sport, via Team Talk)David de Gea

Kipa wa Manchester United, David de Gea

Beki wa Paris St-Germain Thomas Meunier, 27, amekataa kuthibitisha au kukana tetesi kuhusu uhamisho wake kwenda Manchester United au Arsenal mwezi Januari mwakani huku kandarasi yake ikitarajiwa kikamilika msimu ujao. (RTBF, via Mirror)

Mkufunzi wa Real Madrid Zinedine Zidane ameridhishwa na utendajikazi wa Gareth Bale,30, na anaamini mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Wales, akishirikiana vizuri na Eden Hazard, watakua kiungo muhimu kwa   Real Madrid. (ESPN)Gareth Bale

Gareth Bale

Bale amesema anatarajia “misuko suko mingi “kabla ya “uamuzi” kuhusu hatma yake Real Madrid. (Sky Sports)

Kocha wa zamani wa Manchester United Jose Mourinho alikataa kumsaini Virgil van Dijk mwezi Januari 2018, kabla ya mchezaji huyo kujiunga na Liverpool. (Independent, via Liverpool Echo)

Liverpool ni miongoni mwa vilabu vinavyomnyatia vinga wa miaka 20 wa Villarreal na Nigeria Samuel Chukwueze. (Goal)

Inter Milan ilimuulizia kiungo wa kati wa Borussia Dortmund Mjerumani Mario Gotze mwezi Agosti na huenda ikamnunua mshezaji huyo wa miaka 27 Januari mwakani. (La Gazzetta dello Sport)

Juhudi za Tottenham kumsajili kiungo wa kati wa Sporting Lisbon Bruno Fernandes, 24, ziligonga mwamba kutokana “ugumu” wa mfumo wa kuwasilisha ofa, amesema rais wa Sporting Frederico Varandas. Spurs ilikua tayari kulipa £40m kabla ya mkataba kufikiwa na baadae kuongeza £18m ikiwa wangelishinda Ligi ya Premia na Champions League. (Evening Standard)Bruno Fernandes

Kiungo wa kati wa Sporting Lisbon, Bruno Fernandes

Beki wa Derby Krystian Bielik, 21, anasema AC Milan ilitaka kumsajili kabla aondoke Arsenal kwenda Rams. (Derby Telegraph)

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents