Michezo

Tetesi za Soka Ulaya PSG yamuweka Neymar sokoni, Countinho hatiani Chelsea, Mo Salah aikacha madrid na wengine sokoni

Tetesi za Soka Ulaya PSG yamuweka Neymar sokoni, Countinho hatiani Chelsea, Mo Salah aikacha madrid na wengine sokoni

Klabu ya Paris St-Germain ipo tayari kumuuza mshambuliaji wake machachari raia wa Brazil, Neymar, 27. (L’Equipe – in French). Klabu ya Bayern Munich inataka kumsajli kwa mkopo winga wa Real Madrid na timu ya taifa ya Wales Gareth Bale, 29. (Sun). Kiungo wa klabu ya Lyon Mfaransa Tanguy Ndombele, 22, amesema kuwa anaweza kuhamia Tottenham kama nafasi itatokea. (Telefoot – in French)

Manchester United wanamtaka beki wa kulia wa kalabu ya PSV Eindhoven na Uholanzi, Denzel Dumfries, 23. (Sun)

Liverpool wameingia kwenye kinyang’anyiro cha kufukuzia saini ya kiungo wa klabu ya Besiktas na Uturuki, Dorukhan Tokoz, 23. Tayari ofay a klabu ya Udinese ya Italia ya kutaka kumsaini kiungo huyo imekataliwa na Besitkas. (Fotomac – in Turkish)

CoutinhoHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionPhilipe Coutinho amekuwa akihusishwa na fununu za kuhama klabu ya Barcelona

Winger wa klabu ya Barcelona na timu ya taifa ya Brazil Philippe Coutinho, 27, anaweza kujiunga na Chelsea. (Express)

Kipa mkongwe wa Italia Gianluigi Buffon, 41, amesema anaweza kupumzika msimu mzima kucheza mpira baada ya kukataa ofay a kuongeza mkataba kwa mwaka mmoja na klabu ya PSG. (Corriere dello Sport, via Goal)

Gigi BuffonHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionGigi Buffon ametangaza kuachana na klabu ya PSG

Rais wa PSG Nasser Al-Khelaifi ameonya kuwa hataki tena kuona “tabia za watu mashuhuri” kutoka kwa wachezaji wake. (France Football – in French)

Kocha wa Manchester City Pep Guardiola anataka kumsajili kipa wa klabu ya Eibar Mhispania Asier Riesgo, 35. (Sun)

Asier RiesgoHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionAsier Riesgo

Kocha wa Inter Milan Antonie Conte anataka kumsajili mlinzi wa zamani wa Chelsea na England Gary Cahill, 33, baada ya beki huyo kuondoka Chelsea. Cahill na Conte wamewahi kufanya kazi pamoja Chelsea. (Sport Mediaset – in Italian)

Klabu ya Manchester United wamepewa nafasi ya kumsajili kiungo wa klabu ya Monaco Youri Tielemans. Tielminas, 22, ambaye ni raia wa Ubelgiji kuanzia mwezi Januari mwaka huu alikuwa kwa mkopo klabu ya Leicester. (Star)

Youri TielemansHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionYouri Tielemans

Kiungo wa Everton na timu ya ataifa ya Croatia Nikola Vlasic, 21, anajiandaa kuhamia moja kwa moja klabu ya CSKA Moscow baada ya kuitumikia kwa mkopo kwa msimu mzima. (Championat – in Russian)

Watford wanatarajiwa kuingia kwenye kinyang’anyiro cha kumsajili beki wa est Brom dCraig Dawson, lakini klabu ya Burnley imetangaza nia pia ya kumsajili beki huyo mwenye miaka 29. (Sun)

Tetesi Bora za Jumapili

SalahHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES

Mshambuliaji wa klabu ya Liverpool na timu ya taifa ya Misri Mohamed Salah, 27, amekataa ofa ya uhamisho ya pauni 150 milioni kutoka vilabu vya Real Madrid na Juventus. (Mirror)

Kiungo wa Manchester United na timu ya taifa ya Ufaransa Paul Pogba, 26, yupo tayari kuanza mgomo ili kushinikiza uhamisho wake kwenda Real Madrid. (ABC – in Spanish)

United pia wanampango wa kumsajili beki Mfaransa Issa Diop, 22, kwa dau la pauni milioni 45 kutoka West Ham. (Sky Sports)

Harry MaguireHaki miliki ya pichaREX FEATURES

Beki wa Leicester na England Harry Maguire, 26, alikubaliana na mmiliki wa klabu hiyo ambaye sasa ni marehemu Vichai Srivaddhanaprabha kuwa angeruhusiwa kuhama baada ya kukamilika kwa msimu uliopita. (Mirror)

United ambayo inanolewa na Ole Gunnar Solskjaer pia inaonekana kupokwa tonge mdomoni na Barcelona ambao wapo tayari kutoa dau la pauni 150 milioni ili kumng’oa Antoine Griezmann, 28, kutoka klabu ya Atletico Madrid. (Mirror)

Chanzo BBC.

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents