Habari

Thuli Madonsela wa Afrika Kusini ashinda tuzo ya ‘Forbes Africa Person of The Year’

Thuli Madonsela wa Afrika Kusini amefanikiwa kushinda tuzo ya ‘Forbes Africa Person of The Year’ kwa mwaka 2016.
0000214659

Modonsela alitangazwa kushinda tuzo hiyo Alhamisi hii mjini Nairobi huku akikumbukwa zaidi kwa msimamo wake mkali dhidi ya ufisadi alipokuwa anahudumu kama mlinzi wa maslahi ya umma Afrika Kusini.

Baada ya kushinda tuzo hiyo, Thuli kupitia mtandao wa Twitter ameandika, “Thanks @forbesafrica for an awesome evening and everything regarding #POY16.”

Wengine waliokuwa wanawania tuzo hiyo ni pamoja na Rais John Magufuli wa Tanzania, Rais wa Mauritania, Ameenah Gulib, Mwanzilishi wa Capitec Bank na Michiel Le Roux na wengine.

Wafuatao ni washindi wa tuzo hiyo miaka ya nyuma

Mohammed Dewji (Tanzania)– 2015
Aliko Dangote (Nigeria)– 2014
Akinwumi Adesina (Nigeria) – 2013
James Mwangi (Kenya) – 2012
Sanusi Lamido Sanusi (Nigeria)- 2011

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents