Michezo

FA yawapiga marufuku wachezaji wa Uingereza kutoka usiku wakiwa kambini

Wachezaji wa timu ya taifa ya Uingereza, wamezuiwa na chama cha soka cha nchi hiyo FA, kwenda kufanya starehe usiku wakati wakiwa kwenye michezo ya kimataifa.

2111

Chama cha soka Uingereza FA, kimesema kuwa kinatazama madai kuwa wachezaji kadhaa wa timu ya taifa walienda kutembea usiku, baada ya ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Scotland, ambapo siku tatu baadae walikuwa na mchezo mwingine dhidi ya Uhispania, ambapo walitoka sare ya mabao 2-2.

Tayari nahodha wa timu hiyo ambaye pia ni nahodha wa klabu ya Manchester United, Wayne Rooney, ameomba radhi baada ya picha kumuonesha akiwa kwenye harusi moja usiku akiwa amelewa.

Katika hatua nyingine gazeti la The Sun limedai kuwa siku hiyo zaidi ya wachezaji 10 wa timu ya taifa ya Uingereza, walienda kwenye vilabu vya usiku na kunywa pombe hadi alfajiri ya kesho yake.

Uamuzi wa FA ambao haukutokana na kile kilichofanywa na Rooney pekee, haitegemewi pia kama FA itachukua hatua dhidi ya mtu yeyote.

Mkurugenzi mtendaji, Martin Glenn amesema kuwa “Msifanye maigizo kuhusu hili. Tunafanya uchunguzi unaostahili wa kilichotokea. Inasikitisha. Nikitendo kibaya na ameomba radhi. Alichokifanya hakioneshi mfano mwema kwa nahodha wa timu ya taifa, lakini sipendi kiongezwe chumvi.”

“Je kulikuwa na maofisa wa FA waliohusika? Tunatafuta ukweli. Tunaongea na watu ambao walikuwepo kwenye tukio na kama waliwaona. Na vipi ufanye kitendo kama kile wakati unajua sheria kuhusu vilevi kwa wachezaji wa timu ya taifa zinajulikana? Lazima kuna maswali yataulizwa hakika.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents