Burudani

TMK Wanaume Family kuja na wimbo wa Anniversary

TMK Wanaume Family ni moja kati ya makundi yaliyowatoa mastaa ambao bado wanafanya vizuri kwenye muziki mpaka sasa.

fella-1[1]

Ukimya wa miaka kadhaa bila ya kuona wimbo wowote wa kundi hilo na kuibuka kwa Yamoto Band, kumeibua maswali mengi kuwa inawezekana TMK Wanaume Family inaweza ikawa imekufa.

Akiongea na Bongo5, meneja wa kundi hilo Said Fella maarufu kama Mkubwa Fella amesema, ‘wimbo wa kundi upo tayari na baada ya mfungo wa Ramadhan kila kitu kitaenda sawa.’

“Tulitaka kufanya Anniversary ya TMK Family mwaka jana, harakati za uchaguzi zilisababisha tushindwe kufanya. Baada ya mwezi mtukufu wa Ramadhani tutaachia wimbo wa kundi pamoja na kufanya Anniversary kwa pamoja,” ameongeza.

“Kwenye huo wimbo wa kundi pia yupo Aslay na Maromboso. Hatujawaweka wasanii wote wa ‘Yamoto’ kwa sababu ingekuwa ni kama TMK Wanaume Family wamewashirikisha Yamoto Band.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents