Burudani

Hanscana adai director wenye uwezo wa kushoot video kali hapa bongo ni wachache

Mtayarishaji wa video za muziki nchini Hanscana amesema wasanii wanaotaka kushoot video zao hapa nyumbani ni wengi lakini tatizo ni directors wenye uwezo wa kutengeneza video kali ni wachache.
hanscana4

Akizungumza katika kipindi cha Enewz cha East Africa Television Jumanne hii, Hanscana amewakata madirector wenye uwezo kujitokeza ili kuchangamkia fursa hiyo.

“Watu wanaotaka kushoot video ni wengi sana nchini lakini watu ambao wana uwezo wa kutengeneza video kali ni wachache sana, jambo ambalo linafanya kutokuwepo kwa mgawanyo wa kazi,” alimesema Hanscana

Pia Hanscana alisema director bora kwake ni yule anayepimwa kwa wingi wa kazi anazozifanya kwa mwaka kulinganisha na wenzake.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents