HabariSiasa

Trump kuwani urais kwa mara ya tatu

Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump atarajiwa leo kuzindua kampeni yake ya kuwania kiti cha urais kwa mara ya tatu katika wakati anakabiliwa na ukosoaji baada ya chama chake cha Republian kupata matokeo mabaya ya uchaguzi wa hivi karibuni.

Tangazo hilo anatarajiwa kulitoa mnamo alasiri kwa saa za Marekani baada ya hapo jana kutoa ishara ya kufanya hivyo kupitia mtandao wake wa kijamii wa Truth akisema leo “itakuwa moja ya siku muhimu katika historia” ya taifa hilo.

Trump alitumai angeweza kutumia mafanikio ya chama chake katika uchaguzi wa katikati ya muhula uliofanyika wiki iliyopita lakini matokeo ya uchaguzi huo yameonesha wagombea wa chama cha Republican hawakufanya vizuri.

Mwanasiasa huyo alishindwa uchaguzi wa rais wa mwaka 2020 ameendelea kuwa na ushawishi mkubwa ndani ya chama cha Republican tangu alipotoka madarakani.

Related Articles

Back to top button