HabariMichezo

Try Again na Infantino kwenye kozi ya FIFA

Mwenyekiti wa Bodi, Salim Abdallah ‘Try Again’ akisalimiana na Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani (FIFA), Gianni Infantino baada ya kushiriki moja ya vipindi vinavyoendelea kwenye kozi ya Diploma katika Uongozi wa Klabu inayotolewa na FIFA (Diploma in Club Management) inayofanyika mjini Tangier, Morocco.

Try Again ni mmoja wa wajumbe watatu kutoka Afrika ambao wanashiriki kozi hiyo ambapo kwa upande wa Afrika Mashariki alichaguliwa yeye peke yake.

Huu ni mwendelezo wa FIFA kutoa kozi hiyo ambayo ilianzia nchini Qatar wakati Kombe la Dunia likiendelea ambako pia Try Again alishiriki.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents