Burudani

#Tuzozawatu Special: Vanessa Mdee aongelea Coke studio, baadhi ya watu kutoamini uwezo wake na tuzo za watu

Zikiwa zimesalia siku 6 tu hadi kufika siku ya utoaji wa tuzo za watu utakaofanyika June 27, tunakuleta karibu na nominees mbalimbali walioingia fainali, ambao watakueleza kuhusu kazi zilizowafanya watajwe, masuala mengine kuhusu kazi zao na jinsi walivyozichukulia tuzo za watu baada ya kutajwa.

74094_10151111096236572_480537484_n

Leo tumepiga story na Vanessa Mdee aliyetajwa kuwania kipengele cha video ya muziki inayopendwa ya mwanamuziki wa kike.

Kuhusu kama aliwahi kuwaza angefanikiwa hivi kwa kupata mikataba mikubwa ikiwemo kufanya matangazo ya biashara, kushinda tuzo, Kili tour, Coke Studio na mengine

Nilikuwa natarajiwa makubwa lakini haya ni makubwa haswaa. Ukiwa unafanya kazi ya muziki you hope for things to work out, you hope for things to be beneficial. Kwahiyo naona kama taratibu muziki wa Tanzania umebadilika na wasanii wameanza kupewa kipaumbele so I am just happy to do what I love to do.

Kuhusu kuwepo kwa watu waliohisi hatoweza kufika hapo alipo sasa
Mpaka leo wapo wenye mashaka na mimi. Hainikatishi tamaa bali inanipa changamoto kuendelea kuwaprove wrong na kuendelea kufanya kitu kizuri mpaka wale waliokuwa na mashaka na mimi wakubali waseme ‘yeah she is the one’. So I don’t mind a few doubters.

Kuhusu alivyojisikia kuwa amechaguliwa kushiriki kwenye show ya Coke Studio
Aliniambia meneja wangu, Abby. Alinipigia simu akaniambia ‘guess what! we got Coke studio’. I think this year walikuwa wanauliza mashabiki kupitia social media nani wanataka kuwaona kwenye Coke studio. So Team Vee Money, Money Team, Vanessa Mdee fans ndio walikuwa wanafanya kazi zao, I think that worked.

Kuhusu kuingia fainali za tuzo za watu

Kama nilivyoongea hapo mwanzoni kuhusu nguvu ya mashabiki. Hizi tuzo zimethibitisha kwamba mashabiki ni kila kitu kwa msanii. Kuna wasanii wengi Tanzania lakini wangapi wamepata nafasi ya kuwekwa katika hizi category? Wangapi ambao japo mchuano unaendelea ni wangapi wamebaki kwenye category? Sio wengi. Lakini mashabiki wameniwezesha for that I am grateful.

Msikilize zaidi hapa.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents