Burudani

Uchambuzi: Hiki ndicho WCB na Jay Z na Beyonce wanafanana

Mwaka huu Beyonce ametengeneza vichwa vya habari duniani si tu kwa kushtukiza tena kwa album mpya ‘Lemonade’, bali kwa jinsi alivyoamua kuitumia kuelezea kwa mara ya kwanza skendo ya muda mrefu kuhusu matatizo ya ndoa yake na Jay Z.

WCB

Kwenye wimbo wake ‘Sorry’ alizungumzia jinsi ambavyo mume wake (japo hakumtaja) amekuwa akimsaliti kwa kutembea na wanawake wengine. Mstari ‘You better call Becky with the good hair’ uliopo kwenye wimbo huo uliwaweka kwenye wakati mgumu wanawake wawili waliowahi kudaiwa kuchepuka na rapper huyo ambaye jina lake halisi ni Shawn Carter.

Wanawake hao, Rachel Roy na Rita Ora walijikuta wakishambuliwa kwa zaidi ya wiki kwenye mitandao ya kijamii na mashabiki wa Beyonce, Beyhive.

Kwa mtazamo wa kawaida, Lemonade ni album iliyomuabisha sana Jay Z. Na sio kitu cha kawaida kwa mwanaume mwenye nguvu kama Hov kumruhusu mkewe amvue nguo kiasi hicho hata kama kweli alikosea. Lakini kwa familia ya The Carters, kwa muda miaka mingi maisha yao binafsi yamekuwa kitu kinachowaingizia fedha kila siku. Ni kwasababu Jay Z anadaiwa kusikiliza nyimbo zote zilizomo kwenye Lemonade na kuipa go ahead. Infact kuna uwezekano alikuwepo kwenye session nyingi wakati mke wake alipokuwa akirekodi album hii.

Jay alikubali kuimbwa hivyo na mkewe kwa imani iliyotimia kuwa Lemonade ingeingiza mkwanja mrefu na mwisho wa siku wawili hao watajitupa kitandani, kubusiana kwa mahaba mazito na kufurahia champagne ya ghali kwa mkwanja wanaoendelea kuingiza. Hiyo inathibitika kama anavyosema Jay kwenye mashairi ya remix ya Fat Joe na Remy Ma ‘All The Way Up.’

“You know you made it when the fact your marriage made it is worth millions. Lemonade is a popular drink and it still is,” anarap Jay Z.

Na sasa tuje kwenye ufanano wa maisha ya Bey na Jay na label ya Wasafi.

Jumatano hii msanii wa label hiyo, Raymond aliachia wimbo mpya alioupa jina Natafuta Kiki. Wimbo huu una mistari ambayo kwa hali ya kawaida isingekuwa rahisi kwa Diamond kama bosi wake airuhusu ipite.

Ni kwasababu inagusa watu ambao kiuhalisia hawapo sawa na Diamond ama inamkosea heshima. Lakini hii ni showbiz na kujilipua ni sawa na chumvi kwenye mboga. Natafuta Kiki imepewa baraka zote na uongozi wa label hiyo licha ya kuwa na mistari yenye utata.

Hii ni mistari ambayo kwa mtazamo wa kawaida isingekuwa ‘healthy’ uhusiano wa Ray Vanny na bosi wake.

Au niwatukane wote wanaoimba kwa dharau na kuvimba mpaka yule anajiita Simba!

Diamond ni bosi wa Raymond ni heshima hata kufikiria kumtukana? Sio rahisi lakini hii ni showbiz, ruksa kwa kijana huyo kujilipua hivyo na bosi wake amempa green light. Mwisho wa siku ngoma inakiki, jina la Ray linakuwa kubwa, anapata show nyingi, mkwanja unarudi WCB and everyone is happy!

Kiki ipi iko njema, au niende kwa Sepetu Wema?

Tangu waachane kwa mara ya mwisho, Diamond na Wema hawajawahi kuwa na ukaribu wowote, infact kwa jinsi wasivyoelewana na Zari, maisha yao ni kama maji na mafuta. Ray anapata wapi ‘balls’ za kufikiria kwenda kwa Wema?

Nimtongoze Zari, akijua Mondi si hatari?

Zari ni roho ya Diamond kwa sasa hivi kweli hata ile Ray kufikiria kumtongoza mama wa mtoto wa bosi wake si ni ‘abomination’ kwa sauti za waigizaji wa Nigeria?

Nataka nibadili ratiba, kwangu isije leta msiba, Nitoke Wasafi niende kwa Kiba

Si wanasema adui wa rafiki yako ni adui yako pia? Lakini kwanini WCB imemruhusu Raymond imtaje mtu ambaye kwa muda mrefu amekuwa akihusishwa kuwa na bifu na bosi wake? Well, hawa jamaa wanaelewa kuwa baadhi ya vitu havitakiwi kufuatwa kama vilivyo kama unataka kutengeneza pesa kwenye showbiz! Ndio maana amepewa baraka zote kwamba mwisho wa siku Ray kama mtoto hapaswi kujiingiza kwenye tension isiyomhusu. Na huu ndio mstari unaopendwa zaidi kwenye wimbo huu na umeonesha jinsi ambavyo WCB imeamua kuula mfupa ambao kwenye situation kama hiyo ungewashinda wengi.

Kwahiyo mfanano wa Lemonade na Natafuta Kiki ni ule uthubutu wa kutumia maisha halisi kutengeneza hit song. Na sasa ukipita sehemu kibao si ajabu kukuta mashabiki wakiburudika na Natafuta Kiki. Hiyo ndio inaitwa showbiz! Unaweza ingia ucheze sindimba, huwezi kaa pembeni uwaachie wenye ‘balls.’

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents