HabariSiasa

Uganda: Wanaosema Spika Oulanya ameuawa kwa sumu wasakwa

Polisi nchini Uganda wametishia kuwakamata watu wanaodai kwamba laiyekuwa spika wa nchi hiyo Jacob Oulanyah aliuawa kwa kupewa sumu.

Oulanyah aliaga dunia March tarehe 19 2022 akipokea matibabu nchini Marekani baada ya kutibiwa katika hospitali tofauti nchini Uganda na Kenya.

Kufuatia kifo chake, uvumi ulienea nchini Uganda kwamba Oulanyah alifariki kutokana na madhara ya sumu aliyopewa na kwamba sumu hiyo ilikuwa ya mda mrefu mwilini kabla ya kusababisha kifo.

Museveni atoa amri wanaozungumzia kifo cha Oulanya kukamatwa

Rais wa Uganda Yoweri Museveni, alisema baada ya kifo cha Oulanya kwamba “ametoa amri kwa polisi kufuatilia wanaondika kwenye mitandao ya kijamii kwa Jacob Oulanya alifariki baada ya kupewa sumu, na kuwakamata wanaotoa madai hayo ili watoe ufafanuzi na kueleza polisi kile wanachokijua kutokana.”

Lakini familai ya Oulanya, inasisitiza kwamba alipewa sumu.

Wakati wa mazishi yake, baba wa Oulanya Nathan L’Okori, kupitia kwa mkalimani, alisema kwa lugha ya Luo kwamba “nataka walio hapa wote kujua kwamba Oulanyah alipewa sumu. Aliniambia mwenyewe kwamba alipewa sumu. Alifanyiwa upasuaji. Madakatari walijaribu kukabiliana na sumu hiyo lakini tayari ilikuwa imesambaa mwilini. Wakati alisafirishwa kwa ndege kupata matibabu Marekani, alikuwa katika hali mbaya ambayo hangepona.”

Ripoti ya kwanza kuhusu spika kupewa sumu

Mnamo mwezi Agosti mwaka uliopita, gazeti la Observor la nchini Uganda, liliripoti kwamba “rais Yoweri Museveni alikuwa ameagiza timu maalum ya usalama kuchunguza sababu zilizokuwa zikipelekea afya ya Spika Jcaob Oulanyah, ikiwemo madai ya kupewa sumu.”

Wakati wa mazishi ya Oulanya, jumamosi April 8 2022, waziri wa afya wa Uganda Dr. Jane Ruth Aceng, alisema kwamba “Oulanya alifariki baada ya viuongo muhimu mwilini kukosa kufanya kazi. Moyo ulishindwa kufanya kazi, mapafu, ini na kulikuwa na maambukizi katika sehemu kadhaa za mwili.”

Licha ya polisi kushikilia kwamba itawakamata na kuwazuilia wanaosema kwamba aliyekuwa spika Oulanya alipewa sumu, madai bado yanaenea Uganda.

Naibu wa chama kinachotawala asema alijua kuhusu ‘Oulanya kupewa sumu’

Naibu mwenyekiti wa chama kinachotawala cha National resistance movement NRM, Godfrey Kiwanda, ameambia radio ya Capital Fm katika mjadala maalum, Jumapili asubuhi April 9, kwamba Jacob Oulanya, alimwambia kwamba “alikuwa amepewa sumu na kwamba tukio hilo lilifanyika mda mfupi baada ya kuchinda uchaguzi wa kiti cha spika, mwezi May mwaka uliopita 2021.”

Kiwanda, ambaye alikuwa Waziri wa utalii katika serikali ya Museveni, amesema kwamba anaamini kwamba “honi kama kuna ripoti zinazokinzana kati ya madai ya Oulanya kupewa sumu na ripoti ya madaktari katika hospitali ya Marekani, ambayo haikusema kwamba Oulanya alikufa kutokana na viungo muhimu mwilini kukosa kufanya kazi kutokana na ugonjwa wa saratani inavyosema serikali.”

Video ya televisheni ya NTV Uganda, iliyowekwa kwenye mitandao ya kijamii, inaonyesha naibu wa mwenyekiti wa chama kinachotawala cha NRM Godfrey Kiwanda, akisisitiza kwamba “Oulanya mwenyewe akiniambia kwamba alipewa sumu. Hakujua ni wapi alipewa sumu hiyo wala hakuiambia aliyempa sumu. Sasa haya madai ya aliyekuwa spika kupewa sumu hayakuanza a familia yake. Yalianza na Oulanya mwenyewe akiwa hai. Na siwezi kunyamaza kusema ninachokijua. Hata niliambia baadhi ya watu wakati Oulanya alikuwa bado hai.”

Source: Voice Of America

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents