Siasa

Pakistan: Imran Khan aondolewa madarakani

Waziri Mkuu wa Pakistan Imran Khan ameondolewa mamlakani baada ya bunge kupiga kura ya kutokuwa na imani naye.

Washirika wake kadhaa na chama kikuu kwenye muungano na chama chake hawakumuunga mkono kwenye kura hiyo huku wakimlaumu kwa kusabisha kuanguka kwa uchumi wa Pakistan na kushindwa kutekeleza ahadi alizozitoa kwenye kampeni.Pakistan Misstrauensvotum gegen Premierminister Imran Khan

Wanajeshi nje ya Bunge la Pakistan.

Khan awali alijaribu kuzuia kura hiyo kwa kulivunja bunge na kuitisha uchaguzi wa mapema lakini Mahakama ya juu nchini Pakistan iliamuru kura hiyo iendelee. Upinzani ulishinda baada ya wabunge wapatao 174 kupiga kura ya kutokuwa na Imani na Imran Khan. Bunge la Pakistan lina jumla ya viti 342

Spika wa bunge, Ayaz Sadiq alitangaza matokeo mapema leo Jumapili baada ya kumalizika zoezi hilo la kupiga kura lililochukua takriban saa 13. Wabunge wachache tu wa vyama vilivyo katika muungano na chama cha Imran Khan cha Tehreek-i-Insaf au Vuguvugu la Pakistan la Haki waliohudhuria kikao hicho, yeye mwenyewe hakuhudhuria.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents