Habari

Uingereza: Chama cha Conservative chashinda uchaguzi mkuu

Kiongozi wa chama cha Conservative Boris Johnson amewashukuru wapiga kura wa Uingereza kwa kushiriki kwa wingi katika uchaguzi wa mwezi Disemba.

UK Wahlen 2019 | Erste Hochrechnung (Getty Images/AFP/T. Akmen)

Akizungumza na vyombo vya habari muda mfupi baada ya chama chake kushinda zaidi ya viti 326, Boris Jonhson amesema kwamba hatua hiyo inaipatia serikali mpya fursa ya kuheshimu maamuzi ya kidemokrasia ya raia wa Uingereza ili kuliimarisha taifa hilo.

Chama cha Boris Johsnon kilihitaji kujipatia viti 326 ili kutangazwa kuwa mshindi lakini kufikia sasa kimepitisha idadi hiyo na kufikia viti 334.

Chama cha Boris Johnson chashinda kwa ingi wa kura

Chama cha Boris Johnson chashinda kwa wingi wa kura

Waziri huyo mkuu amesema kwamba uamuzi huo unampatia jukumu la kufanikisha Brexit na kuiondoa Uingereza katika muungano wa Ulaya.

”Zaidi ya yote nataka kuwashukuru watu wa taifa hili kwa kujitokeza kupiga kura ya Disemba ambayo imebadilika na kuwa ya kihistoria, ambayo inatupatia sisi kama serikali mpya fursa ya kuheshimu uamuzi wa kidemokarsia wa raia wa kulibadilisha taifa hili na kuonyesha uwezo wa raia wa taifa hili”.

Hatua hiyo inajiri muda mchache baada ya mpinzani mkuu wa Boris Jonson Jeremy Corbyn kusalimu amri na kusema kwamba hatokiongoza tena chama hicho katika uchaguzi mkuu ujao.

Uamuzi huo wa kiongozi wa Leba unajiri huku chama hicho kikikabiliwa na matokeo mabaya zaidi ya uchaguzi katika miongo kadhaa.

Chama cha Conservative kimeshinda baadhi ya viti katika ngome za chama cha Leba.

Chama cha Leba kimepoteza viti kaskazini mwa England , Midlands na Wales yakiwa ni maeneo yaliopiga kura ya Brexit katika kura ya maoni ya 2016.

Leba inatarajiwa kushinda viti 61 ikiwa ni chini ya viti ilivyoshinda 2017 imedaiwa.

Baadhi ya maeneo bunge kama vile Darlington ama Workington , kaskazini mwa England yataongozwa na mbunge wa Chama cha Conservative kwa mara ya kwanza katika miongo kadhaa- ama katika matukio ya Bishop Auckland na Blyth Vally kwa mara ya kwanza tangu viti hivyo kubuniwa.

Lakini Leba kimeshinda kiti cha eneo bunge la Putney, kusini magharibi mwa London kutoka kwa Conservative.

Chama cha Uskochi cha kitaifa kimepata ushindi wake wa kwanza usiku wa kura , kikishinda eneo bunge la Rutherglen na Hamilton magharibi kutoka kwa chama cha Leba na Angus kutoka kwa Conservative.

Matokeo hayo ambayo yanatoka katika vituo 144 vya kupigia kura yameimarishwa ili kuangazia matokeo rasmi.

Imebainika kwamba Conservative watapata wabunge 357 ikiwa ni wabunge 39 zaidi ya uchaguzi wa 2017 kura zote zitakapohesabiwa.

Chama cha Leba kitajipatia wabunge 201, SNP wabunge 55 , LIberal Democrats 13, Plaid Cymru 4 The Greens 1 brexit Party 0.

Huku matokeo ya maeneo bunge 175 yakiwa yametangazwa , ongezeko la wastani katika kura ya chama cha Conservative ni asilimia 2 ikiwa ni pointi moja ya kilichotarajiwa katika kura hiyo.

Kura ya chama cha Leba ilipungua kwa asilimia 9 kulingana na utabiri wa matokeo ya kura hiyo yasio rasmi.

Nchini Uskochi, kumekuwa na ongezeko la asilimia 9 katika chama cha kitaifa cha Uskochi – ikiwa ni kiwango cha chini ya ilivyotabiriwa kwa asilimia 13 lakini SNP kinaelekea kushinda viti 55.

Waziri wa maswala ya ndani wa chama cha Conservative Priti Patel alisema kwamba serikali itahakikisha kwamba Brexit inafanyika kwa haraka kabla ya Christmas kupitia kuwasilisha miswada iwapo serikali yake itarudi mamlakani.Priti Patel

Waziri wa maswala ya ndani wa chama cha Conservative Priti Patel alisema kwamba serikali itahakikisha kwamba Brexit inafanyika kwa haraka kabla ya Christmas

Mbunge wa zamani wa Conservative Sir Alan Duncan ambaye amekuwa mkosoaji mkubwa wa Boris Johnson amesema kwamba waziri mkuu huyo sasa ndiye mwanasiasa mwenye umaarufu mkubwa Uingereza na kwamba uchaguzi huo umethibitisha hilo.

Aliambia BBC ”sasa tutaweza kutawala kwa wingi wa kura”.

Mgogoro ulikuwa tayari umezuka katika chama cha Leba kuhusu ni nani anayefaa kulaumiwa katika kile kinachotarajiwa kuwa uchaguzi wake mbaya zaidi katika miongo kadhaa.

Mwenyekiti wa Leba Ian Lavery ambaye alihifadhi kiti chake kwa uchache wa kura alizopata awali amesema kwamba amesikitishwa akisema kwamba wapiga kura katika ngome za chama cha Leba wanaomboleza kuhusu msimamao wa Brexit wa chama hicho.

Chansela kivuli John McDonald aliambia BBC kwamba matokeo ya kura yasio rasmi yalikuwa yanasikitisha kwa Leba.

”Nilidhania ushindani utakuwa wa karibu mno” , alisema na kulaumu kile alichokitaja kuwa uchaguzi wa Brexit, wakati Leba ilitarajia kwamba maswala mengine yatachipuka.

Alimwambia mwandishi wa BBC Andrew Neil kwamba uamuzi utafanywa kuhusu kiongozi wa chama hicho Jeremy Corbyn katika siku za usoni wakati matokeo rasmi yatakapotolewa.

Shughuli ya kuhesabu kura UingerezaHaki miliki ya pichaAFP
Image captionShughuli ya kuhesabu kura Uingereza

Baadhi ya wagombea wa Leba wamekosoa uongozi wa Corbyn .

Gareth Snell ambaye alisema kwamba alitarajia kupoteza kura ya Stoke Central kwa chama cha Conservative alimtaka bwana Corbyn na bwana McDonald kuondoka lakini pia akawalaumu wanachama wa chama hicho wanaopinga Brexit kwa kukisukuma sana chama hicho.

Afisi ya waziri mkuu katika taarifa yake imesema kwamba iwapo matokeo hayo yasio rasmi yatathibitishwa na Johnson kurudi uongozini kutakuwa na mabadiliko machache ya baraza la mawaziri siku ya Jumatatu.

Muswada wa makubaliano ya kujiondoa utakaorahisisha kuondoka kwa Uingereza tarehe 31 Januari utasomwa kwa mara ya pili katika bunge tarehe 20 mwezi Disemba.

Mabadiliko makubwa ya baraza la mawaziri yatafanyika mwezi Februari , baada ya Uingereza kuondoka EU huku taarifa ya bajeti ikitolewa mwezi Machi.

Kufanikisha Brexit

Huu ni uchaguzi wa Uingereza wa tatu chini ya miaka mitano na wa kwanza kufanyika mezi Disemba katika kipindi cha miaka 100 na umetawaliwa na kura ya maoni ya 2016 ya kuondoka katika muungano wa Ulaya.

Bwana Johnson aliangazia ujumbe mmoja- kuhakikisha Brexit inafanikiwa- akiahidi kuiondoa Uingereza katika EU kufikia tarehe 31 mwezi Janurai 2020 iwapo angepata wingi wa kura.

Chama cha Leba kilifanya kampeni ya kuongeza matumizi katika huduma za umma mbali na katika vituo vya afya.

Chama cha Liberal Democrats kiliahidi kufutilia mbali Brexit iwapo kiongozi wake Jo Swinson angechaguliwa kuwa waziri mkuu , lakini kura ya maoni ilitabiri kwamba ufuasi wao utapungua wakati wa kampeni.

Chama cha kitaifa cha Uskochi kilisema kwamba uungwaji mkono wao utaashiria kura ya maoni ya pili kufanyika.

Kiongozi wa SNP Nicola Sturgeon alituma ujumbe wa twitter kwamba huku matokeo hayo yasio rasmi yakiashiria kwamba ulikuwa usiku mzuri kwa chama hicho , aliongezea kwamba kile kinachoonekana kuwa ‘kikubwa ni kidogo’.

Caroline Lucas ambaye matokeo hayo yanaonyesha kwamba anatarajiwa kuwa mbunge wa pekee wa chama hicho cha Green Party , alituma ujumbe katika twitter akisema: iwapo matokeo haya ni ya kweli basi ni pigo kubwa kwa hali yetu ya hewa kwa kizazi kijacho na demokrasi yetu.

Nigel Farage alisema kwamba chama hake cha Brexit kilipata kura kutoka kwa Leba katika maeneo bunge yaliolengwa na chama cha Consercative ijapokuwa yeye mwenyewe aliharibu kura yake kwa kuwa ‘nisingeweza kukipigia kura chama cha Conservative’.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents