HabariSiasa

Ujerumani kuboresha uhusiano na Afrika

Waziri wa biashara wa Ujerumani Robert Habeck afanya ziara nchini Namibia na Afrika Kusini ili kujaribu kukuza uhusiano wa karibu na nchi hizo mbili katika sekta ya nishati.

Habeck atasafiri leo Jumapili kuelekea Namibia na kisha Jumatatu jioni ataelekea Afika Kusini ambapo anatarajiwa kuzuru mji wa Cape Town, Johannesburg na Pretoria kwa zaidi ya siku tatu.

Miongoni mwa agenda zake, Habeck analenga kuboresha uhusiano wa kiuchumi na kupendekeza mkutano wa kilele wa biashara kati ya Ujerumani na Afrika.

Related Articles

Back to top button