Habari

Ukimaliza kupiga kura, rudi nyumbani – Rais Uhuru Kenyatta

Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta ametoa wito kwa wapiga kura nchini humo kuondoka kwenye vituo vya kupigia kura mapema baada ya kumaliza zoezi hilo.

Tokeo la picha la uhuru kenyatta
Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta

Kiongozi huyo ametoa wito huo katika hotuba kwa taifa kabla ya uchaguzi mkuu kesho Jumanne Agosti 8 2017 nchini humo., kwa wananchi wanafaa kupiga kura kwa amani.

“Ombi langu ni kwamba tunapopiga kura, hebu tupige kura kwa amani na tukumbuke kama nilivyosema jana, kwamba baada ya kupiga kura yako, nenda nyumbani. Nenda kwa jirani yako, bila kujali anatoka wapi, kabila lake, rangi au dini, jirani yako ni ndugu yako, Jirani yako ni dadako, Jinsi ulivyopiga kura haifai kwa vyovyote vile kuathiri au kubadilisha jinsi unavyohusiana na jirani yako Msalimie kwa mkono, kuleni chakula pamoja na uwaambie ‘hebu tusubiri matokeo’ kwani Kenya itaendelea kuwepo kwa muda mrefu hata baada ya uchaguzi”,amesema Rais Kenyatta kwenye hotuba yake kwa Taifa.

Taarifa kutoka nchini humo zinadai muungano wa upinzani (NASA) ulikuwa awali umewashauri wafuasi wake kutoondokakwenye vituo vya kupigia kura baada ya kupiga kura ili kulinda kura zisiibiwe, Lakini baadaye, muungano huo ulibadilisha wito wake na kuwashauri waondoke baada ya kupiga kura.

Hata hivyo, Polisi wamewataka wananchi nchini Kenya kuheshimu sheria ya kutokuwa karibu na vituo vya kupigia kura kwa umbali wa mita 400 baada ya kupiga kura.

By Godfrey Mgallah

 

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents