Habari

Waziri Lukuvi akabidhi hatimiliki 88

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. William Lukuvi amekabidhi hatimiliki 88 kwa wakazi wa Kimara, jijini Dar es Salaam ambapo hati 4333 ambazo ziko kwenye hatua za mwisho katika mradi wa urasimishaji wa makazi holela.

Akikabidhi hatimiliki hizo, Mhe. Lukuvi amesema hizi hati ni mtaji uliofufuliwa baada ya wakazi kukakaa na kuendeleza maeneo yasiyopimwa yaani mtaji mfu kwani hakuna mtu yeyote ambaye angewezakupata mkopo bila hati.

“Kwa hati hizi zilizotolewa takribani 4333 tukisema kila nyumba ikopeshwe kwa kiwango cha chini cha shilingi milioni 10, kwa siku ya leo Kimara inapata mtaji wa karibu bilioni 40.5,” alisema Lukuvi.

Mhe. Lukuvi amesema kuwa Serikali ya Aawamu ya Tano inayo dhamira ya dhati ya kurasimisha makazi nchi nzima ili kuongeza thamani ya ardhi au maeneo husika. Ardhi yenye hatimiliki thamani yake inaongezeka kwani inatambuliwa na taasisi za fedha ambazo ni rahisi kukopesha wenye hati.

Na Emmy Mwaipopo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents