Michezo

Ulevi wamtia mbaroni Roberto Firmino

Mchezaji wa klabu ya Liverpool Roberto Firmino ameshtakiwa kwa kosa la kuendesha gari akiwa mlevi baada ya kukamatwa mkesha wa siku ya Krismasi.

Mshambuliaji huyo ambaye ana umri wa miaka 25 alikamatwa baada ya gari lake kusimamishwa katikati mwa Liverpool mapema siku ya Jumamosi ,polisi wamesema.

Firmino amabye ni raia wa Brazil anatarajiwa kufikishwa mbele ya hakimu wa Liverpool mnamo Januari 31. atawasilishwa mahakamani siku ambayo timu yake itakuwa ikikaribisha Chelsea katika uwanja wa Anfield.

Liverpool ilimsajili kutoka Hoffenheim kwa kandarasi ya miaka mitano iliogharimu kitita cha pauni milioni 29 mwezi Juni.

Liverpool imesema kuwa haitazungumzia swala hilo hadi pale hatua hiyo ya kisheria itakapokamilika.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents