Burudani

Unakumbuka ile story kuwa Hussein Machozi alifumaniwa na mke wa mtu Mombasa? Huu ni ukweli kutoka kwake (Audio)

Waingereza wanasema ‘bad news spreads fast and far’, yaani kwamba habari mbaya husambaa haraka na mbali. Pengine Hussein Machozi ni mmoja wa watu wanaoweza kuuelezea vyema usemi huu.

hussein

Unakumbuka ile habari kuwa muimbaji huyu alifumaniwa akiwa na mke wa mwanasiasa maarufu nchini Kenya ilivyosambaa? Ni kweli jamaa alifumaniwa? Machozi ameutoa uhondo wote kwenye Chill na Sky.

“Kuna dada mmoja wasanii watakuwa wanamjua sana, huwa anaandaa show, alinitafuta, alisikia nimeenda Mombasa, akaniambia njoo Sarova hapa, hoteli moja babkubwa sana. [Nimeenda], nimemkuta yeye yupo kwenye swimming, kwahiyo mimi nikawa nimechill out namsubiri atoke tuendelee kuzungumza,” amesimulia Hussein.

[Ghafla niliona zimeingia gari mbili nyeusi na watu fulani wameenda juu kama sita saba hivi. Mzee basi full kupigwa makofi ‘kaa chini, fanya hivi.’ Yule dada ananiambia ‘kimbia’ sasa nikimbie nimefanya nini? Sasa wakati mzozo huo umeendelea wamenikalisha chini, ile gari ya pili sasa akashuka jamaa ambaye mimi simjui, wanasema ni mwanasiasa mkubwa mimi nilikuwa sielewi,” ameongeza.

“Wakati anashuka jamaa sasa aje kuniface, kuna gari nyingine tu ya kawaida, Vitz ikamshusha mwanamke mmoja hivi mama ambaye ndio mke halisi wa huyo jamaa. Kwahiyo huyo mama akawa kama amekuja kunisaidia mimi kwasababu ilibidi amshike mashati jamaa ‘umekuja kufanya nini hapa.’ Ugomvi ukawa kati ya yule mwanamke aliyeniita mimi na yule mama, kwamba wenyewe ndio wamefumaniana. Yule jamaa alivyoona vile akaamuru watu wake wapande kwenye ndinga wasepe waepuke kizazaa kipya tena ambacho kimezaliwa. Wale wahudumu wakaniambia ‘bwana sepa, ruka kwenye fensi ya beach. Mimi nikaruka upande wa beach nikachepuka. Sasa walioanza kusambaza habari kwamba Hussein amefumaniwa ni wale wahudumu wa ile hoteli.”

Unaweza kusikiliza kipindi kizima cha Chill na Sky hapo chini.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents