Habari

Upinzani waongoza kura za urais Zambia

Mgombea mkuu wa upinzani nchini Zambia anaongoza wakati kura zikiendelea kuhisabiwa kufuatia uchaguzi uliokuwa na ushindani mkali kati yake na rais aliyepo madarakani, Edgar Lungu, anayelalamikia uchaguzi kuharibiwa kwenye majimbo matatu muhimu kwake.

Kufuatia idadi kubwa ya watu kujitokeza kwenye upigaji kura wa siku ya Alhamis, Hakainde Hichelema hadi jioni ya jana (Jumamosi, 14 Agosti) alikuwa anaongoza wakati asilimia 40 ya kura zikiwa zimeshahisabiwa.

Hadi hapo, Tume ya Uchaguzi ya Zambia (ECZ) ilikuwa imeshatangaza matokeo ya majimbo 62 kati ya 156, ambapo Hichelema alikuwa mbele kwa kura 1,024,212 dhidi ya Lungu aliyekuwa na kura 562,523.

Awali, waangalizi wa Umoja wa Ulaya walikuwa wamesema kwamba kampeni za uchaguzi huo hazikuendeshwa kwa haki na kwamba mamlaka zilitumika kumpendelea Rais Lungu.

Hii ni mara ya tatu kwa Hichelema kupambana na Lungu katika kile wachambuzi walichotabiri kwamba ungelikuwa mchuano mkali kutokana na malalamiko ya kupanda kwa gharama za maisha na ukandamizaji wa dola dhidi ya wapinzani.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents