Michezo

USAJILI: Yanga SC yapata mbadala wa Msuva

Mabingwa wa kihistoria wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara klabu ya Yanga imemsajili winga wa kimataifa wa Burundi, Baruan Yahya kwa mkataba wa miaka miwili na akitarajiwa kuchukua nafasi ya Mtanzania, Simon Msuva anayetimkia nchini Morocco.

Winga wa kimataifa wa Burundi, Baruan Yahya

Mchezaji huyo raia wa Burundi amesema kuwa anafurahishwa na uwezo wa wachezaji waliyo sajiliwa na Yanga SC.
“Nafurahishwa na uwezo wa wachezaji, Thaban Kamusoko na Ibrahim Ajib wanavipaji vya hali ya juu na uwezo wao unanipa kiu ya kufanya makubwa msimu ujao”.Amesema Baruan Yahya.

Mpaka sasa kikosi hicho cha Mzambia, George Lwandamina kina jumla ya wachezaji watano, kipa Mcameroon, Youthe Rostand aliyesajiliwa kutoka African Lyon, beki Abdallah Hajji ‘Ninja’ kutoka Taifa Jang’ombe, kiungo Pius Buswita kutoka Mbao FC, na mshambuliaji Ibrahim Ajib kutoka kwa mahasimu, Simba SC.

By Hamza fumo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents