Burudani

Vanessa Mdee anavyojiongezea thamani kwa uwekezaji mkubwa kwenye muziki wake

Wikiendi hii nilikuwa ninaongea na msanii mkubwa wa Bongo Flava, akaniambia ‘Video ya Niroge ya Vanessa itawapa wakati mgumu sana wanamuziki wa kike wa Afrika Mashariki.’

929083_1742128615999680_103982942_n

Alimaanisha kuwa video ya wimbo huo ni kali mno kiasi ambacho kwa wanamuziki wenye akili timamu lazima iwanyime usingizi. Ni kwasababu showbiz kwa sasa imetawaliwa na ushindani na usipokubali kushindana, kaa pembeni, uwapishe wenye nguvu.

Nguvu inayozungumziwa hapa ni ya uwekezaji. Uwezekaji hapa si wa maneno au majungu, ni wa fedha tu. Kwahiyo ili kusurvive kwenye kizazi kipya cha showbiz ya Afrika kwa sasa, inabidi uwe na fedha, utake, ustake. Fedha hii inaweza kuwa yako unayopata kwa shows na biashara zingine au kwa kudhaminiwa na wale wenye nazo. Haijalishi inatoka wapi, ukweli unaoumiza wasanii wengi kwa sasa ni kwamba muziki unahitaji uwekezaji mkubwa – period!

Vanessa Mdee ni mfano wa wanamuziki walioamua kujilipua na kuwekeza fedha nyingi katika muziki wake. Tuseme ukweli, ukiambiwa uweke video 10 kali za Afrika zilizotoka hadi sasa, Niroge haiwezi kukosa. Ni video bora, haijawahi kufanywa na msanii wa Tanzania (kwa maana ya graphics, mavazi, wazo na vitu vingine). Ni zile video ambazo utaziona zikifanywa na akina Nicki Minaj au Katy Perry tu. Ni video inayoiongezea thamani brand ya Vanessa Mdee.

Na kizuri siku hizi hakijifichi. Reaction za kwenye mitandao ya kijamii zinasema yote. Video na wimbo huu vimepata mrejesho chanya uliomshangaza mwenyewe. Mrejesho kama huo humpa moyo msanii kubwa uwekezaji wake haujapotea bure. “My friends ( fans ) are the best. Super positive and encouraging I seriously am feeling the love. God bless y’all,” alitweet Vee.

Ukiangalia graph ya Vanessa kimuziki inapanda kadri siku zinavyoenda. Rudi nyuma kwa kuangalia video za Come Over, Hawajui, Nobody But Me, Never Ever na sasa Niroge, utagundua kuwa Vanessa anashidana mwenyewe.

Wakati akiendelea kuupgrade kazi zake, thamani yake inazidi kupanda. Promoter wa ndani au wa nje anapotaka kuongea na Vanessa kwaajili ya show yake, na akiangalia uwekezaji aliouweka, ni lazima ajifikirie mara mbili.

Akipandisha gharama zake za kufanya show, ina make sense kwa uwekezaji anaoendelea kuufanya. Brand au makampuni makubwa yakitaka kumpa endorsement, ni lazima yaweke kichwani thamani yake ilipo sasa kutokana na vigongo kama video ya Niroge.

Tuwaombee pia wasanii wengine wengi wa kike wapate nguvu hii ya kuwekeza kwenye muziki wao na hata wakifanya hivyo uwekezaji urudi wapate moyo wa kuendelea tena.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents