Burudani

Video: Chris Brown asema atampa ‘high five’ Rihanna kama akisikia ni kweli ana uhusiano na Leonardo DiCaprio

Kumekuwepo na tetesi kwa siku kadhaa sasa kuhusu Rihanna kuwa na uhusiano na muigizaji Leonardo DiCaprio, baada ya wawili hao kuonekana pamoja mara kadhaa katika mazingira yanayoshawishi kuamini uvumi huo.

Chris Brown ana kitu cha kusema kuhusiana na tetesi hizo.

Baada ya Breezy kuulizwa kwenye mahojiano na kituo cha radio Hot 97 jana kuhusu tetesi za ex wake Rihanna kuwa na uhusiano na DiCaprio, alisema yeye hana wivu na atampa ‘high 5’ kama akisikia ni kweli Riri ana uhusiano na muigizaji huyo.

“High five. You had to go up, and that’s the upper, upper echelon. I’m not even a hater. I’ll give you a slap on the back, booty, everything… ‘Hey, do your thing. Good game.'” Alisema Brown aliyeongozana na Tyga kwenye mahojiano hayo.

Breezy aliendelea kusema,

“In that situation, I just tip my hat. I’m not a hater. I’m not envious. I don’t feel jealous… I’m like, do your thing. I can’t have it all, brotha. I can’t have it all.”

Breezy na Tyga walikwenda kwenye mahojiano hayo kuipromote album yao ya pamoja ‘Fan Of A Fan 2’ ambayo imepangwa kutoka leo Feb 24.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents