Burudani

Video: Diva anunua ugomvi wa Vanessa Mdee na Baby Madaha

Mtangazaji wa kipindi cha Ala Za Roho cha Clouds FM, Diva The Bawse ameamua kuununua kwa bei rahisi ugomvi wa Vanessa Mdee na Baby Madaha.

Mara kadhaa Baby Madahga amekuwa akisikika kwa kusema Vanessa ni msanii ambaye anabebwa ndio maana kila tuzo anazoshiriki za nje anakuwa haibuki mshindi – Kauli hiyo imeonekana kumgusa Diva na kuamua kumpa makavu msanii huyo.

Akiongea na Bongo5, mtangazaji huyo amesema, “ Sasa Baby Madaha kweli wakujifananisha na Vanessa kweli? Namfahamu lakini Yule siyo wakujifananisha na Vanessa, atafute level yake ya kujifananisha nao. No disrespect, am not try disrespect her lakini yule asijifananishe kabisa na Vanessa, Vanessa ni hard working you can see, ana focus yeye yule ana focus nini?”

“Yaani anamzungumzia hivyo Vanessa yeye katoa nyimbo gani ambayo atleast watu wanaijua au kafanya video au kafanya kolabo na huyu. Mimi nahisi Baby Madaha sawa sawa na wale wa page hizo za udaku, you can’t compare Baby Madaha na Vanessa, Shout out to Vee Money,” ameongeza.

Mwezi uliuopita Baby Madaha alipokuwa akiongea katika kipindi cha 180 Power cha Sibuka FM, alisema, “Tunapeleka watu kuwania tuzo wengine hawana vigezo vya hizo tuzo, especially nazungumzia kwa madada kuna dada mmoja yaani kila tuzo anaendaga lakini ashindi kutokana na nini hana qualification za hizo tuzo.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents