Burudani

Harmonize amkingia kifua Zari

Baada ya watu kuhoji vipi Baby Mama wa Diamond Platnumz, Zari The Boss Lady anajiachia ile mbaya akila bata wakati ni siku kadhaa tu zimepita tangu afiwe na Mama yake mzazi, Harmonize ameamua kumteta Zari.

Harmonize ambaye naye walikuwepo katika bata hilo Mombasa nchini Kenya, amesema mtu akipata matatizo halafu akapelekwa sehemu nzuri kwa ajili ya kufurahi ni kitu cha kumshukuru Mwenyenzi Mungu.

“Kwa sababu haikuwa rahisi, unajua kufiwa na mazazi sio kitu kidogo. Tumefika (Mombasa) tumemkuta yupo fresh, yaani kasharidhika na matokeo kwa sababu anajua hakuna binadamu atakuja kuishi milele,” ameiambia XXL ya Clouds Fm na kuongeza.

“Kwanza ukiona mtu anazungumza hiyo ujue haijui dini, kwa sababu dini imeandika kila mtu atakufa, kifo ni kitu cha lazima, ukiwa unaijua dini huwezi kuhofia suala la kifo. Mtu kafariki ni lazima uumie ila ni lazima maisha mengine yaendelee kwa sababu hata ukae ndani miaka sita hawezi kurudi,” amesema Harmonize.

By Peter Akaro

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents