Videos

Video: Kimbunga adai Nay wa Mitego alimkosea heshima, ndio maana aliachia ‘Natuma Salamu’

Rapper Kimbunga amesema Nay wa Mitego alimkosea heshima baada ya kumwambia atamshirikisha kwenye ngoma yake ‘Salam Zao’ lakini baadaye akamkacha na kuamua kuitoa mwenyewe.

Kimbunga ameiambia Bongo5 kuwa kwakuwa alikuwa ameshaandika verse yake, aliamua kuongeza nyingine na kurekodi version yake aliyoipa jina ‘Natuma Salamu’.

“Nay wa Mitego alikuwa anataka kunishirikisha kwenye ile ngoma ya Salam Zao, kwahiyo akanifanya mimi nikaandika lyrics, kwasababu mimi nilishafanya naye ngoma zaidi ya tatu, nilishafanya naye Itafahamika tu remix, nilishafanya naye ‘Nasema Nao’ Remix, kwahiyo Salam Zao alikuwa anataka tufanye kama official sasa,”amesema Kimbunga.

“Like end of the time nikaisikia ile ngoma iko hewani. Tayari mimi nilikuwa nipo na mdundo alinipa kwaajili ya kuandikia,” aliongeza.

“Nafikiri ni disrespect aliyokuwa amenifanyia,kwahiyo ni haki yake pia.”

Kimbunga amesema kwa muda mrefu amekuwa akifanya hip hop ya maana lakini watu hawaonekani kujali, na sasa ameamua kufanya ile aliyoiita ‘Hip Hop Drama’.

“Sasa hivi tunachanana tu, ngoma zote zinazokuja sasa hivi za Kimbunga ni michano baada ya michano. Ukipita tu hivi kidogo mimi nakuchana.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents