Burudani

Video: M2 The P kurudi kivingine, Jodan na Mirror wapo pia

Msanii wa muziki Bongo M2 The P ametangaza kurudi kivingine katika game pamoja na Mirror na Jodan.

Mirror na Jodan ambaye walikuwa chini ya usimamizi wa Marehemu Ngwea wamekuwa kimya kwa muda sasa, hata hivyo M2 The P ambaye alikuwa karibu na Ngwea ameeleza kuwa wasanii hao siku siyo nyingi watasikika upya.

“Kwa hiyo soon watu wakae mkao wa kula kazi zinakuja na vizuri zaidi nipo pale kwa Mr. T  Touch nina ngoma nyingi sana na Mr. T” M2 The P ameiambia Bongo5.

“Wapo wadogo zangu, unajua tatizo usimamizi wa kazi, unajua kama usimamizi wa kazi unayumba na wewe lazima uyumbe, walikuwa chini ya usimamizi wa Endless Fame hapa katika kukatokea matatizo lakini kuna ngoma tayari washafanya pamoja na video kwa hiyo watu wangoje” ameongeza.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents