Burudani

Video: Meneja na mke wa Mabeste, Lisa apanga kuwakutanisha mastaa wa kike kwenye mchezo wa ‘Rede’

Kama wewe ni msichana una miaka zaidi ya 25 kwa sasa na enzi za utoto wako hukuwahi kucheza mchezo wa ‘Rede’, utakuwa ulikosa starehe kubwa.

Rede ni mchezo waliokuwa wakicheza wasichana ambapo wawili hukaa huku na kule na mmoja kuwa katikati akijitahidi kuijaza chupa mchanga huku akikwepa mpira anaopondwa na wawili hao.

Meneja na mke wa rapper Mabeste, Lisa Karl Fickenscher amesema anataka kuurudisha mchezo huo kwa kuandaa tamasha litakalohusisha mastaa mbalimbali wa kike na mashabiki wao.

“Rede ni mchezo tuliokuwa tunacheza sisi wadada enzi tulipokuwa mateenagers,” Lisa ameimbia Bongo5. “Lakini sasa hivi mtu na familia yake wako busy na kazi. Kwahiyo nikaona ni mchezo ambao watu wameumiss lakini hawana hiyo nafasi ya kucheza.”

Amesema atatoa nafasi kwa mashabiki wa mastaa mbalimbali kushindana kwenye mchezo huo na washindi watashinda kombe watakalompa staa wanayemkubali na kisha kukutana naye kwa chakula cha pamoja.

Amedai kuwa usaili wa kujiunga na mechi hiyo umepangwa kufanyika Jumapili hii. Mtazame zaidi hapo juu akifafanua.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents