Burudani

Unapenda kufahamu collabo ya Joh Makini na Davido imefikia wapi? Joh afunguka

Kama unawasiwasi juu akiba ya collabo za kimataifa alizonazo John Simon Mseke a.k.a Joh Makini, ondoa hofu kwasababu ile collabo yake na nyota wa Nigeria, David Adedeji Adeleke a.k.a DaVIDO imeshaingizwa kwenye computer ya studio ya The Industry.

joh davido

Davido anamkubali sana Joh Makini, na alithibitisha hilo September 18, 2015 alipovujisha taarifa ambayo muda wake ulikuwa bado, kuhusu yeye na rapper wa ‘Don’t Bother’, Joh Makini kufanya collabo.

Bongo5 ilipomtafuta Joh Makini wakati huo kuzungumzia juu ya collabo hiyo alisema kuwa walikuwa bado hawajarekodi, bali walikuwa kwenye maandalizi, na kuongeza kuwa Davido aliwahi kuiweka wazi.

davido-Joh

Ijumaa hii kupitia XXL ya Clouds Fm, Joh Makini amesema kuwa tayari Davido amesharekodi sauti zake na yeye ameshafanya sehemu zake hivyo muda muafaka ndio unaosubiriwa ili waweze kufanya video na kuiachia single hiyo.

“Ngoma ishapigwa , jamaa kaishafanya yake na mimi nimefanya yangu” alisema Joh.

Hiyo ni ishara nyingine kuwa mwaka 2016 utaendelea kuwa wa mafanikio kwa Joh Makini, ambaye anaumaliza vizuri 2015 kwa collabo iliyopokelewa vizuri sana na mashabiki wa Tanzania, Afrika Kusini na maeneo mengine ya Afrika.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents