Habari

Video: Mwana FA athibitisha kukutwa na Virusi vya Corona ”Inaudhi”

Msanii wa muziki wa hip hip, Mwana FA athibitisha kukutwa na Virusi vya Corona, hii ni muda mchache tu kupita tangu meneja wa Diamond Platnumz, Sallam SK kuweka hadharani majibu yake kuwa na yeye ameathirika.

Kupitia mtandao wake wa kijamii wa instagram FA amethibitisha hilo huku akiwapa moyo Watanza juu ya hali yake na kuwataka kuchukua tahadhari.

”Ndugu  Majibu ya vipimo vyangu vya Covid 19 yamerudi chanya. Inaudhi. Siumwi KABISA. Nipo sawa 100%. Na nimejitenga toka niliporudi ili kuepuka kuathiri wengine. Na kwa bahati hata watoto wangu sijakutana nao kabisa. Hawapo nyumbani.” Ameandika Mwana FA.

Mwana FA ameongeza ”Nawaomba tu tuchukue tahadhari kwa kadri ya uwezo wetu kukwepa usitupate na hata tukipatwa nao sio tatizo la kivile hata,virusi wake wanaondoka wenyewe baada ya siku kadhaa tu. So yah,sisi wa nchi hizi tulioandamwa na migonjwa mikubwa mikubwa katika kukua kwetu,haya ‘mafua’ wala sio kitu cha kututisha. ITAKUWA TU SAWA. Tuweni na amani tu mioyoni.”

Mapema hii leo Meneja wa msanii mkubwa nchini Diamond Platnumz ambaye ni Sallam SK amekiri kukutwa na virusi vya corona na anaendelea kufuata ushauri wa wataalamu wa afya.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents