Habari

Video: Mwanamke alia mbele ya Rais Magufuli akielezea kesi ya mirathi

Mwanamke mjane alijikuta akilia kwa uchungu mbele ya Rais Dkt John Magufuli, kuelezea kero anazozipata kuhusu kesi ya mirathi wakati wa siku ya maadhimisho ya siku ya sheria yaliyofanyika kwenye viwanja vya mahakama, jijini Dar es Salaam.

Mwanamke huyo mkazi wa Tanga, Sobha Mohammed alizua tafrani baada ya kuibuka mara tu Rais alipomaliza hotuba yake akiwa na bango, lakini kabla ya kufika mbele ya meza kuu alikumbana na rungu la walinzi wa Rais.

Mama huyo alirejeshwa nyuma kuondolewa eneo hilo huku watu waliokuwapo hapo wakishuhudia, na wakati huo Rais Magufuli alikuwa katika mazungumzo na Kaimu Jaji Mkuu, lakini baada ya muda mfupi kulitokea agizo la Rais la kutaka aachwe na apelekwe kwao atoe kilio chake.

Alipofika mbele, mama huyo alianza kutoa kilio, na akielezea madhira ya kudhulumiwa haki zake katika kesi iliyofunguliwa mkoani Tanga na kwamba amefika katika ofisi mbalimbali za wahusika wa masuala ya kisheria kuanzia Polisi hadi kwa Waziri wa Katiba na Sheria, Dk Harrison Mwakyembe.

Baada ya kumsikiliza mama huyo, Rais Magufuli aliagiza, “Ofisi ya DPP, AG na Jaji Kiongozi si ndio msimamizi wa kesi zote za chini chini, si ndio bwana. Shughulikie suala la huyu mama. Kama kesi iko Mahakama ya Mwanzo kule muivute huku haraka haraka, ishughulikiwe haraka.”

“Na AG pia mshughulikie, lakini na pia mumlinde ili asidhuriwe kwa kifo cha aina yoyote. Chukua jina lake, lakini pia mtafutieni polisi ili amlinde. Lakini mhakikishe usalama wake. Jaji Kiongozi chukua simu yake. Na mama njoo uchukue simu ya Jaji Kiongozi, umpigie moja kwa moja.”

https://youtu.be/3hX_Vtng2gc

Na Emmy Mwaipopo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents