Habari

Rais hajawahi kutangaza kufutwa kwa vyama vya upinzani- Waziri Mkuu

Waziri mkuu, Kassim Majaliwa amesema kuwa Rais Dkt John Magufuli hajawahi kutangaza au kutoa kauli ya kufutwa kwa vyama vya siasa nchini.

Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo Alhamisi hii, Mjini Dodoma, alipokuwa akijibu swali la mbunge wa Hai, Freeman Mbowe. Swali lake lilikuwa linasema kuwa, Rais Magufuli alinukuliwa akisema kuwa ifikapo mwaka 2020 vyama pinzani vitakuwa havipo. Sambamba na kujiamini kusema kama akileta ushahidi huo, Mbowe alimtaka waziri mkuu kujiuzulu, ndipo Naibu Spika wa Bunge aliingilia kati kwa ajili ya taratibu za bunge. Pamoja na hilo Mbowe alitaka kujua kuhusu kunyimwa dhamana kwa mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema.

Waziri Mkuu amesema kuwa suala la dhamana ni suala ambalo lipo chini ya sheria huku akisema hawezi zungumzia suala hilo.

“Kwanza naomba nikanushe kuwa Rais Magufuli hajawahi kutangaza kuvifuta vyama pinzani,” alisema Majaliwa.

“Watanzania wanajua nchi hii inaendeshwa kwa kanuni sheria na taratibu. Pia Watanzania wanajua kwamba jambo lolote ambalo lipo mahakamani haliwezi kuzungumziwa mahali pengine popote , hivyo siwezi kuzungumzia mambo yoyote ambayo yapo chini ya sheria na yaliyo mahakamani.”

Na Emmy Mwaipopo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents