Michezo

Video: Ronaldo afunguka kuhusu bao lake awashukuru mashabiki wa Juventus

Mshambuliaji wa klabu ya Real Madrid, Cristiano Ronaldo amefunguka kuhusu bao lake la pili alilofunga dhidi ya Juventus mchezo wa klabu bingwa barani Ulaya uliyopigwa mwanzoni mwa wiki hii huko nchini Italia na kumalizika kwa ushindi wa mabao 3 – 0.

Walichokiandika Rashford,Crouch na Ferdinand kuhusu bao la Ronaldo dhidi ya juventus

Ronaldo amesema kuwa  goli hilo linalojulikana kama ‘Scopion kick’ au ‘bicycle kick’ linamfanya kuwa na kumbukumbu kubwa kwenye maisha yake ya soka na kuwashukuru mashabiki wa klabu pinzani ya Juventus kwa kumshangili wakati alipofunga bao hilo kwakuwa hata yeye amekuwa na mapenzi na ushabiki wa Juve tangu angali mdogo.

 

Ronaldo ameisaidia Real kutanguliza mguu mmoja mbele kuelekea hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo ya klabu bingwa Ulaya huku akitarajiwa kuiwezesha kupata matokeo mazuri kwenye mchezo wa marudiano huko nchini Hispania.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents